ULEGA: NCHI ZA ZINAZOZUNGUKA BAHARI YA HINDI KUNUFAIKA NA MRADI MKUBWA WA (SWIOFC) KUTOKANA NA MAZAO YA BAHARI

Waziri wa Mifugo na Uvuvi , Mh Abdallah Ulega amesema Tanzania na nchi nyingine zinazozunguka bahari ya hindi, zinakwenda kunufaika na mradi mkubwa WA mazao ya bahari  pamoja na Samaki unajulikana  kama (SWIOFC).

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano maalum wa wakuu na wataalamu mbalimbali Kutokana na Sekta ya bahari na uvuvi ulionyika  leo 4.12.2024 jijini Dar es salaam ukiwa unawakutanisha wadau kutoka mataifa ya jumuiya ya nchi za Afrika mashariki

Ulega amesema “Mkutano huo umekuja wakati sahihi baada ya kuombwa na nchi wanachama jumuiya hiyo hivyo kutokana umuhimu wake Tanzania imeona  Kuna haja ma  fursa kadhaa zikiwemo mazao yatokanayo na bahari”

Aidha Waziri Ulega amesema hii ni mara ya pili kwa Tanzania kufanya uwekezaji kwenye Sekta Uvuvi katika vyanzo vyake ikiwemo maziwa ambapo amesema “Tumejenga mialo ya kupakulia kusafisha samaki kwenye maeneo yanayozunguka bahari ya Hindi.

Pembezoni na mkutano huo wakuu na wataalamu wa mazao ya bahari wamepata muda wakubadilishana mawazo na utaalamu na uzoefu katika kuendelea Sekta hiyo.


Kwa upende wake,Katibu mkuu wa SWIOFC,Dismas Mbabazi amesema Mkutano huo utaleta matokeo chanya kwa nchi wanachama, ambapo amesema fursa zitapatikana kwa wavuvi na wadau wanaozunguka bahari ikiwemo kukuza uchumi WA mtu mmoja mmoja mataifa Yao kwa ujumla amesema Mbabazi.


Powered by Blogger.