Na Jumanne Magazi
5.11.2024
Dar es salaam
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt Suleimani amemuagiza katibu mkuu wa wizara hiyo kufatilia changamoto za kisheria na kanuni zitafutiwe ufumbuzi ili kuhakikisha sekta ya biashara inakuwa nchini.
Waziri Jafo ametoa maagizo hayo leo Desemba 5, 2024, wakati wa maadhimisho ya kitaifa ya siku ya ushindani duniani, aidha waziri Jafo pia amesema kuwa serikali ya awamubya sita inaboresha miundo mbinu ili kuhakikisha sekta ya Biashara inakuwa kwa kasi ili kuongeza ushindani halili wa bidhaa na masoko katika masoko ya kitaifa.
katika hatua nyingine Waziri Jafo ameagiza mijadala yote itakayojadiliwa katika maadhimisho hayo iwazirishwa kwake ndani ya siku kumi na nne ili kufanyia kazi mawazo yaliyojadiliwa kwa lengo la kuongeza kasi ya ukuaji wa biashara na ushindani wa bidhaa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa tume ya FCC Dkt Aggrey Mlimuka amesema kuwa kuwa tume hiyo inawajibu na kusimamia uwepo wa fursa sawa kwa washindani wakubwa na wadogo katika soko, pia kupunguza ukiritimba katika masoko kwa kuhakikisha washindani wakubwa hawawazuii washindani wadogo kukua na kuingia au kuwatoa sokoni.
kila ifikapo December 5 kila mwaka Dunia huadhimisha siku ya ushindani Duniani ampapo kwa Tanzania maadhimisho hayo yamefanyika jijini Dar es salaam ambapo kaulimbiu katika maadhimisho hayo ni "Sera ya ushindani na kudhibiti kukosekana kwa usawa katika uchumi"
Post a Comment