SAMIA: AWALILIA WAHANGA WA AJALI KARAGWE ATAKIA NAFUU MAJERUHI

Nimepokea kwa masikitiko taarifa za ajali ya barabarani iliyohusisha magari matatu katika Kijiji cha Kihanga, Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera, na kupelekea vifo vya watu saba na majeruhi tisa.

Ninawapa pole familia, ndugu, Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mheshimiwa Fatma Mwassa, jamaa na marafiki. Ninawaombea kwa Mwenyezi Mungu marehemu wote wapumzike kwa amani, na majeruhi wote wapone kwa haraka.

Nimelielekeza Jeshi la Polisi kuhakikisha kuwa madereva wanaongeza umakini na kuzingatia sheria za barabarani hasa kipindi hiki cha mwisho wa mwaka ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika. 

Utekelezaji wa agizo hili uende sambamba na uhuishaji na uwekaji wa alama za barabarani kwenye maeneo hatarishi, pamoja na kuzingatia umbali na maeneo sahihi ya uwekaji wa vituo vya ukaguzi ili vionekane kwa urahisi zaidi. 

Kwa abiria na watumiaji wote wa barabara, nawakumbusha kutumia namba za simu za Makamanda wa Polisi wa Mikoa kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi, wakati wowote wanapoona viashiria vya uzembe na ukiukwaji wa sheria na alama za Barbara ni 


Powered by Blogger.