TTB: YAPELEKA TUZO ZAKE ZA DUNIA KILELE CHA MLIMA KILIMANJARO

Na Jumanne Magazi 

5.12.2024

Dar es salaam 

Katika kuadhimisha kumbukumbu ya Miaka 63 ya Uhuru wa Tanganyika, Bodi ya Utalii Tanzania - TTB kupitia Kampeni ya “TWENZETU KILELENI” inapeleka Tuzo za ubora katika paa la Afrika, Tuzo zilizotolewa na World Travel Award, TTB imeshinda kama Bodi Bora Barani Afrika kwa miaka mitatu mfululizo.

Aidha TTB imekuwa mshindi kuanzia mwaka (2022,2023 na 2024), zoezi hili linachangizwa Wafanyakazi wa TTB wakiwemo akina Mama waliojitoa kwa dhati ili kuendelea kuunga mkono jitihada za mwongoza watalii nambari moja Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinara wa mafanikio ya Utalii Tanzania.

Hii ni sifa kwa Tanzania na ni faharikwa bara zima la Afrika kwani imekuwa ikitangaza vivutio vyake kwenye majukwaa ya Kimataifa.

 

Powered by Blogger.