TAKUKURU ILALA: YATAHADHARISHA VITENDO VYA RUSHWA KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA KESHO J,TANO

Na JUMANNE MAGAZI 
26.11.2024
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rishwa, Mkoa wa Ilala TAKUKURU imesema imejipanga kuhakikisha inazuia dalili na viashiria vyote vinavyohusu  Rishwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini, dar es salaam mkuu wa Takukuru mkoa wa kikazi ilala, sosthenes Kibwengo amesema wao kaka TAKUKURU ILALA,wamewomba Wananchi wote kuhakikisha wanachagua viongozi kutokana sifa ma sera zao.


Kibwengo amesema “ tunajua kuwa Hila na mbinu wakati WA Uchaguzi hazikosekani lakini wao kama Taasisi wamejipanga kupambana na viashiria vyote kabla wakati na baada ya Uchaguzi”

Aidha Kibwengo amesema kwa muda mrefu wamekuwa Wakitoa elimi kwa Wananchi kujua na kukataa madhara ya Rushwa, hivyo amekemea wagombea mawakala na mashabiki kuepuka vitendo vya Rushwa kwani watakabiliana na mkono WA Sheria.
Katika hatua nyingine Kibwengo ametoa Rai kwa Wananchi kujitokeza kupiga kura siku ya Uchaguzi, na kutekeleza haki  yao ya kikatiba bila hofu,kwani Serikali pamoja na vyombo vya ulinzi vimejipanga kuhakikisha Uchaguzi unafanyika katika hali ya Amani na utuliviu.

Katika hatua nyingine Kibwengo amekumbusha kuwa kura ni Siri na kwa mujibu wa utaratibu uliozoeleka kura ni Siri hivyo Wananchi wasikubali kushawishiwa kuingia kwenye mtego wowote WA kutoa au kupokea Rushwa kwa minajiri ya kumchagua Mgombea yoyote iwe kwa masilahi ya mgombea au chama chake au yeye binafsi.


Vilevile Kibwengo amewaasa viongozi na wanasiasa kuacha kufanya kampeni wakati siku ya Uchaguzi pamoja na kutoa ahadi zilizo na viashiria vya Rushwa kwani atakayebainika, hatua Kali zitachukuliwa dhidi yake.

Powered by Blogger.