TIGO:YABADILISHWA JINA SASA HABARI YA MJINI NI "YAS"

Na Jumanne Magazi 

26.11.2024

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Jerry Silaa (Mb),

Waziri wa Miundombinu, Mawasiliano na Usafirishaji – Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mheshimiwa Dr. Khalid Salum Mohammed, Leo Novemba 26.11.2024, wamekuwa sehemu ya uzinduzi wa Jina la kampuni ya Mawasiliano ya  YAS ,ambayo umefanyika jijini dar es salaam.

Akizungumza wakati wa Uzinduzi huo,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Jerry ameipongeza kampuni hiyo kwa uwekezaji iliyofanya ambapo amedai huo ni muelekeo mzuri katika Sekta ya Biashara hususani Mawasiliano.

Silaa amesema awali TIGO imekuwa ikifanya vizuri jambo ambalo limekuwa likichangia ukuaji WA Pato la Taifa, huku akishahuri kampuni mpya ya YAS kufuata nyayo na yale yote yaliyokuwa yakifanywa na watangulizi wao.

Awali mkuu YAS MIX, Bi Angelika Pesha amesema "Ni heshima kubwa kusimama mbele yenu leo katika tukio hili ambalo linaashiria hatua muhimu katika safari yetu ya utoaji huduma za mawasiliano na za kifedha hapa nchini. Napenda kumshukuru kila mmoja wenu kwa kujumuika nasi katika tukio hili lenye dhamira ya kujenga mustakabali bora kwa Watanzania wote.

Aidha Pesha amesisitiza kuwa Tigo tumekuwa na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa Uchumi wa nchi yetu, tukiwa miongoni mwa makampuni 30 yanayoongoza kulipa kodi hapa Tanzania tukichangia kiasi cha trilioni 1.08 kwa kipindi cha miaka mitatu kama kodi ya VAT, tozo, PAYE na kodi ya zuio. 

Vile vile, Pesha amesisitiza kuwa "Tigo tumetoa mchango mkubwa kwenye ajira. Tunatoa ajira za moja kwa moja kwa watanzania zaidi ya 600 na zile zisizo za moja kwa moja takribani 200,000 kupitia wabia wetu wa mauzo waliosambaa nchi nzima. Tunawekeza vilivyo kuhakikisha tunanoa vipaji vya wafanyakazi wetu na kuwawezesha kutoa huduma bora kwa wateja wetu zaidi ya milioni 23 nchi nzima.      

Pesha amesema kuwa Sekta ya mawasiliano imekuwa kiungo muhimu kwenye sekta mbalimbali pamoja na kuwa na mchango chanya kwenye maendeleo ya jamii na ukuaji wa Uchumi hapa nchini. 

Katika hatua nyingine Pesha amedai kuwa Kwa miaka 30 tuliyotoa huduma za kibunifu hapa Tanzania, safari yetu imejaa hadithi za ubunifu unaoendana na mahitaji ya wateja. Chapa ya Tigo, Tigo Pesa zimekuwa moja kati ya chapa zinazoaminiwa na Watanzania.

"Tumeboresha miundombinu ya mawasiliano ambapo sasa tuna zaidi ya minara 4,000 yenye teknolojia ya 4G kote nchini na 5G katika miji mikubwa. Hii imetufanya kuwa kinara wa ubora wa mawasiliano hatua iliyotambuliwa na taasisi za kimataifa na kitaifa"


 

Powered by Blogger.