MAKUYUNI WILDLIFE PARK KUFUNGUA NJIA YA MAFURIKO YA WATALII

 
Na Beatus Maganja, Arusha.

 MAMLAKA ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) imeanza rasmi utekelezaji wa mikakati ya kuiendeleza na kuiandaa  Hifadhi ya Makuyuni Wildlife Park iliyopo Mkoani Arusha Kwa ajili ya kupokea wageni wengi zaidi kwa kuongeza mindombinu ya utalii hususani barabara, ujenzi wa mabwawa ya maji Kwa ajili ya wanyamapori na kuondoa mimea vamizi ndani ya eneo hilo.

Hayo yamesemwa leo Novemba 24, 2024 na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TAWA Dkt. Simon Mduma katika ziara ya wajumbe wa Bodi hiyo ya kukagua ujenzi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na TAWA ndani ya Hifadhi ya Makuyuni Wildlife Park
"Hifadhi hii ni mpya ilikabidhiwa takribani mwaka mmoja uliopita na katika mchakato wakuiendeleza na kuiandaa Kwa ajili ya kupokea wageni kulikuwa na umuhimu wa kuongeza barabara kwenye maeneo haya ili wageni watakaokuwa wanatembelea eneo hili wawe na wigo mpana wa kuiona mandhari nzuri sana ya eneo hili lakini vilevile kutoa nafasi kubwa ya kuona vivutio ambavyo vipo kwenye hifadhi hii" amesema Dkt. Mduma

"leo tumezunguka na tumeona maendeleo ya ujenzi wa barabara, ni kazi ambayo inaridhisha, ni nzuri na ratiba ambayo ipo kwa makubaliano kwenye  mikataba Kazi ya ujenzi wa barabara inaendelea vizuri sana hilo tumeridhika nalo" ameongeza" Mduma.
 utaanza hivi karibuni kwakuwa mikataba imekwisha sainiwa tayari Kwa kuanza kazi hiyo.

Dkt. Mduma amesema kutokana na eneo la Makuyuni kukumbwa na changamoto ya ukame wakati wa kiangazi kiasi cha kusababisha wanyamapori kutoka nje ya hifadhi hiyo na kwenda kwenye makazi.ya watu, Bodi ya TAWA iliona umuhimu wa kujenga bwawa la kukusanyia maji Kwa ajili ya wanyamapori, hivyo Bodi hiyo imefanya ukaguzi wa eneo litakapochimbwa bwawa hilo na kuridhishwa nalo, na hivyo ujenzi wake utaanza hivi karibuni kwakuwa mikataba imekwisha sainiwa tayari Kwa kuanza kazi hiyo.
TAWA, Makuyuni Wildlife Park ya miaka mitano ijayo  haitakuwa kama inayoonekana leo badala yake itakuwa Makuyuni yenye mabadiliko makubwa ambayo inafungua njia kwa watalii wengi zaidi lakini pia Makuyuni yenye utofauti mkubwa na maeneo mengine yenye vivutio vya utalii.

Naye Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi ambaye pia ni Kaimu Kamanda wa Uhifadhi Kanda ya Kaskazini ya TAWA Privatus Kasisi amesema Kitendo cha Serikali kuiamini TAWA na kuikabidhi eneo hilo muhimu  kumeipa chachu na nguvu ya kuliendeleza na kulisimamia kwa ukamilifu ili kulifanya liwe bora kwa manufaa ya wakazi wa Mkoa wa Arusha na Taifa Kwa ujumla.

Aidha Kasisi amesisitiza kuwa TAWA itahakikisha inaongeza kasi ya uboreshaji wa miundombinu ya eneo hilo ili kupata watalii wengi na mapato kwa muda mfupi hasa katika mashindano ya AFCON ya mwaka 2027 ambapo Tanzania inatarajia kupokea wageni wengi kutoka mataifa


Powered by Blogger.