TIGO: YAKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI WA” MAGIFT YA KUGIFT KWA WIKI YA PILI

Na Jumanne Magazi 

22.11.2024

Kampuni ya mtandao wa Mawasiliano ya Tigo, Leo hii imekabidhi zawa mbalimbali kwa washindi 7 washindano la “Magift ya kugift” ambao wamejishindia kiasi cha TSh Milioni Moja kila mmoja pomoja na simu za mkononi kwa washindi wawili.

Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo, Meneja Bidhaa wa Tigo Eginga Mohamed amesema anayofuraha kukabidhi hii ni sehemu ya utaratibu wao kutoa zawadi mbalimbali ikiwemo pesa taslimu na zawadi nyinginezo.

Eginga amesema mpaka sasa wameshatoa zawadi za fedha zenye thamani ya  kiasi cha  TSh milion 24 kwa washindi wa makundi kada tofauti ikiwemo mawakala,na wateja wengine.
Kwa upande wake Mwanaraph Muhidini ambaye amejishindia simu ya mkononi “amemshukuru tigo kwa zawadi hiyo kwani siku chache zilizopota amepotelewa na simu”hivyo amewataka watuwaendelea kutumia huduma za tigo 
Naye Ramadhan Idd mkaazi WA kinondoni ambaye ameshinda zawadi ya TSh Milioni Moja amemshukuru kupata pasa hizo ambapo amesema atazitumia kwa ajili ya ada ya shule kwa watoto wake.
Kwa upande wao mawakala Mercy Joseph ambaye ni mshindi wa million Moja ametaja sababu kilichomsaidia kushinda ni kutokana kufanya sana muamala hususani kwa upande wa huduma ya lipa kwa simu mara nyingi.

Hii ni wiki ya pili kati kati ya wiki 12 ambazo Tigo kupitia msimu huu wa siku kuu Tigo umepanga kutoa zawadi Zaidi kupitia kampeni Yao ya Magift ya kugift kwa mwaka huu wa 2024.


 

Powered by Blogger.