Waziri Aweso: ameagiza DAWASA wafufue visima vya maji


 NA  JUMANNE MAGAZI ( ILALA ) 30.09.2024

Waziri wa Maji Juma Aweso, ameagiza DAWASA ifufue visima vya maji ili wananchi waweze kutumia maji ya visima kuondoa changamoto za maji kwa wananchi. 

Waziri wa Maji Juma Aweso, alisema hayo Mtaa wa Mafuriko Ilala Bungoni wilayani Ilala wakati wa kuzindua mradi wa maji wa

 Jumuiya hiyo uliojengwa na Serikali ya Mtaa kwa ajili ya Wananchi wa Bungoni katika mkutano ulioandaliwa na Ally Shauri Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Nafuriko.

"Siwezi kuwa kikwazo kwa wananchi wa Jimbo la Ilala wasipate maji ya visima moja ya sifa ya Kiongozi utaonekana kwa vitendo ukishiriki ya watu watashiriki ya kwako anayelala na mgonjwa ndio anajua sifa zake Kanuni zimetungwa na Waziri watazibadilisha nitatoa maelekezo DAWASA itatue  kero kwa jamii watu wapate maji ya Visima" alisema Waziri Aweso

Waziri Aweso alitumia fursa hiyo kumpongeza Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Mafuriko Ilala Ally Mshauri na Jumuiya yake ya Maji ambapo alichangia shilingi Milioni 1 kuwaunga mkono .

Aidha alisema maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kutatua kero za wananchi hivyo nitakikisha wananchi wanapata huduma ya maji safi na salama .

Alitumia fursa hiyo kumpongeza Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu kwa utendaji bora wa kazi na kujituma kwa wananchi kwani Mbunge Zungu ni sehemu ya Chuo Kikuu kwa viongozi vijana wanaochipukia wengi wanaofuata nyayo za Mbunge Zungu wanafanikiwa.

Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu ambaye ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akisema jimbo la Ilala kuna mafanikio makubwa ya miradi ya maendeleo ikiwemo sekta ya afya na sekta ya Elimu na Miundombinu ya Barabara ni sehemu ya kazi ya Serikali ya Dkt samia suluhu Hassan.

Mbunge Zungu alisema Rais amefanya makubwa katika jimbo la Ilala miradi mikubwa ya maendeleo imetekelezwa ikiwemo Reli ya kisasa SGR Bwawa la Umeme Mwalimu Julius Nyerere na Jimbo la Ilala wamepata miradi mikubwa ikiwemo sekta ya afya na sekta ya Elimu na Miundombinu ya Barabara 

Powered by Blogger.