TPDC YATOA UFAFANUZI TAHARUKI KUKOSEKANA KWA MUDA GESI ZA MAGARI DAR
Na Jumanne Magazi
3.0ct.2024
Dar es salaam
Shirika la maendeleo ya Mafuta ya Petroli na Gesi Nchini TPDC, limetoa ufafanuzi kuhusu hitilafu iliyojitokeza kwenye vituo vya kutokea huduma ya gesi asilia kwenye Magari maarufu (CNG).
Akizungumza na Waandishi wa habari mapema hii Leo Oktoba 3, 2024, Kaimu Mkurugenzi mkuu wa TPDC, Mhandisi Emanuel Gilbert amesema kufuatia kutokea hitilafu ya Umeme kwa vitoa dada vya kutolea huduma hiyo hususani kituo cha Uwanja wa ndege na Kituo cha Tazara ambavyo ni vituo dada vilisitisha huduma hiyo kwa Zaidi ya saa 22 jambo lililosababisha usumbufu mkubwa kwa wateja na watumiaji WA huduma hiyo. Aidha Gilbert, wametoa wito kwa Wananchi kuendelea kuwa watulivu na kuacha kusikiliza taarifa zisizo Rasmi ambazo zimekuwa zikisambazwal ambazo nyingi si za ukweli wowote
Vilevile amedai kuwa TPDC kwa sasa shirika Lina mikakati kabambe ya muda mrefu na mfupi ili kutanua huduma na miundo mbinu hiyo ya gesi asilia (CNG).
Post a Comment