TAASISI SELAM YA SWEDEN IKISHIRIKIANA NA TARO, KUIWEZESHA BAJETI YA SANAA NA UTAMADUNI NCHINI

Katika kuhakikisha inakuza Sekta ya Sanaa na. Utamaduni nchini SERIKALI imeombwa kuongeza bajeti kwa asilimia ya moja ya bajeti kuu ya serikali kwenye sekta ya sanaa na utamaduni ili kukuza sekta hiyo

Wito huyo umetolewa leo mapema jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi mtendaji wa Taasi ya haki ya Wasanii,Tanzania Arts Rights Organization(TARO),Wakili Joshua Msambila,wakati wa kikao cha kitaifa cha kujadili namna bora ya kuongeza uwekezaji wa serikali kwenye sekta ya utamaduni kikao cha kitaifa ni sehemu ya mradi unaondeshwa na Selam Wakishirikiana na umoja wa Afrika chini ya ufadhili wa serikali ya Sweden,

Wakili Msambila amesema kwa sasa sekta ya utamaduni inamchango mkubwa kwa maendeleo ya Taifa ikiongezewa fedha inaleta tija zaidi

"Tunataka fedha iongezwe kwasababu fedha inayowekwa ni kidogo sekta ya sanaa inahitaji miundombinu,inahitaji ulinzi pamoja na kuwekeza kwenye Biashara"Amesema Wakili Msambila 

Wakili Msambila k  amesema sekta ya sanaa inamchango mkubwa  kwenye sekta ya uchumi inahitaji uwekezaji wa kifedha ili kuleta tija zaidi.

Kwa upande wake Balozi wa Sweden Tanzania Bi Charlotta Ozaki Marcia's amesema ushirikiano huu utaleta tija kuwa baina ya Taasisi Selam ambayo Iko chini ya ufadhiri WA Serikali ya Sweden katika kukuza ukuaji WA Sanaa na utamaduni kwa kuongeza fedha kwenye bajeti ya Wizara ya Sanaa utamaduni na michezo ambapo imeonekana kuwa kuwa na asilimia ndogo ukilinganisha na michezo.

Aidha amesema wao kama Serikali wanawajibu kukukuza  Taasisi zilizo chini ya Serikali kuendeleza miradi ya kisekta.

Kwa upande wake Bi Beatrice Waruinge - ambaye  ni afisa mshahuri wa mrdi WA selem amesemAdvocacy Program Officer

Selam, Connect for Culture Africa amesema Taasisi Yao imekuwa na miradi hapa barani afrika ikijulikana kama Pan African international Organization, amesema moja ya miradi iliyochini ya selem pamoja na Pan African for artists freedom na Connection  Curture (PANAF). 

Ambapo amesema Jukumu lao kubwa ni kusimamia viongozi wa Serikali za nchi za Africa kutekeleza kwa wakati na kusimama Mazingira mazuri ya kazi za Sanaa na wasanii ili kuwasaidia wasanii ili wanufaike na Kazi zao bunifu kisekta.




 

Powered by Blogger.