MWALIMU NYERERE ALIYAISHI MAISHA YA ZAMA ZOTE :WARIOBA
Akizungumza na wanahabari Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba ameyasema hayo nyumbani kwake wakati akizungumza na wanahabari maswala mbalimbali yanayohusu Taifa na jamii kwa ujumla.
Aidha katika hatua nyingine Warioba pia amezungumzia hali ya kisiasa Nchini pamoja na uongozi wa RAIS Samia Suluhu Hassan pamoja na falsafa yake ya 4R.
Warioba amesema hayo leo Oktoba 4,2024, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam, na kwamba kwa sasa nchi imetulia kisiasa tofauti na miaka mitatu iliyopita.
Amesema changamoto za kisiasa ni kama kuna mapambano kwa serikai na wapinzania ambao hawawasilishi hoja ipasavyo, huku akishauri wanasiasa kukaa meza moja kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
“Amani inajengwa na wananchi wenyewe na sio polisi, kwasababu hata tulipopata uhuru hatukutumia mtutu wa bunduki bali kwa amani.Polisi wanaposikia maandamano yametangazwa alafu wanasema wanalinda amani wajifakari kwa kuwa ulinzi wa nchi unatokana na wananchi wenyewe bila kujali taasisi moja,”amesema.
Post a Comment