ONGEZENI UFANISI WA UBUNIFU MAJENGO KWA MASLAHI YA NCHI: TBA


 Na Jumanne Magazi 

29.10.2024

Hatimaye Serikali imewataka wataalamu wa ubunifu wa majengo na ukadiriaji majenzi kuwa weledi kazini badala ya kuangalia maisha yao binafsi ya kujipatia fedha kwa muda mfupi.

Kauli hiyo imetolewa leo Oktoba 29, 2024 Jijini Dar es salaam na Mkuu wa Wilaya ya Ilala , Edward Mpogolo akimwakilisha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Dotto Biteko katika Mkutano wa tano wa Bodi ya wabunifu wa Majengo na Wakadiriaji Majenzi.

Hata hivyo DC Mpogolo amesema Serikali ipo kwenye mchakato wa kufanyia maboresho sera ya Ujenzi ili kukuza sekta ya mabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi kufanya kazi kwa ufanisi na miradi ya ujenzi wanayopatiwa na Serikali na sekta binafsi kukamilika kwa wakati.

"Baadhi ya wataalamu wa ubunifu wa Majengo na ukadiriaji Majenzi wamekua wakiangalia maisha yao binafsi kwa ajili ya kujipatia fedha kwa muda mfupi huku suala la weledi kazini likiwa limewekwa pembeni hali ambayo inasababisha majengo kuwa chini ya kiwango.

Amesema kwasasa serikali ipo kwenye mchakato wa kufanyia maboresho sera ya ujenzi ili kutengeneza Sheria ya ujenzi itakayosaidia wataalamu hao kufikia matamanio ya kukuza sekta ya ujenzi kutokana na mabadiliko ya teknolojia yanayoenda kwa kasi Duniani.

“Jitihada zinazopatikana katika sekta ya ujenzi inatokana na nyinyi wataalamu wa ubunifu wa Majengo na ukadiriaji Majenzi,ukiona mafanikio yaliyopo kwa sasa yanatokana na nyinyi,hivyo kwa niaba ya serikali nawaomba sana muwe Wazalendo ili tumuunge mkono Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan” amesema DC Mpogolo.



Powered by Blogger.