INFINIX NA TIGO WAZINDUA SIMU JANJA HOT 50 SERIES NA HOT 50I.
29.10.2024K
Kampani ya Infinix Tanzania ambao ni wauzaji WA simu za mkononi hii Leo Oktoba 29 2024 ikishirikiana na kampuni na mtandao wa simu za mkononi ya Tigo Tanzania imezindua toleo jipya ya simu janja aina ya Hot 50 Series na Hot 50i.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huyo Meneja wateja maalum na Vijana Kutoka Tigo, Ikunda Ngoi amesema kampuni Yao inayofuraha na fahari kuwa sehemu ya ushirikiano na Infinix hususani kwenye mabadiriko ya teknolojia ya Simu janja, ambapo ameipongeza Infinix kwa kuleta simu janja inayokwenda na wakati ikiwa imesheheni ubora Mkubwa kwa sasa sokoni ukilinganisha na simu nyingine.
Aidha Ngoi amesema simu ya Hot 50 Series ni nzuri na rahisi kwa matumizi yote hususani kwa manzania wa kawaida na inampa machaguo mengi kwenye ulimwengu WA kidijiti.
Vilevile Ngoi amefafanua kuwa tayari Infinix imeshaingiza sokoni matokeo ya aina tatu yakiwa na ofa mbali mbali Kutoka Tigo ikiwemo pia mteja atajipatia bando la data, na ofa nyingine mbalimbali.
Katika hatua nyingine Ngoi ameendelea kufafanua kuwa simu ya Hot 50 Series. Imekuja na mabadiriko mengi ikiwa na ukubwa WA Gb 128, RAM 8 ambapo mbali na mambo mengine mteja atakayeinunua atapata bando la GB96 Bure.Kwa upande wake Meneja bidhaa WA Infinix Bi. Lilian Mbabala amesema bidhaa Yao hiyo ya Hot 50 Series imekuja kuleta mapinduzi mengine kwenye ulimwengu WA simu janja hivyo wameingiza sokoni simu iliyo na ubora UFANISI mkubwa hivyo amewataka wateja na watanzania kununua simu hiyo ili wajionee tofauti.
Aidha amesema simu Hot 50 Series, inakata na chaji muda mrefu, pia Ina kamera Kali, kioo kikubwa, mteja ataweza kucheza games mbalimbali kuangalia video bila kugandaganda na pia ni toleo la jipya la Kasi ya 5G, hivyo mteja ataweza Kunitumia bila usumbufu wa kugandaganda, hii ni faahari nyingine Kutoka kampuni ya Infinix.
Post a Comment