TIRDO, REPOA KUJA NA MRADI WA MATUMIZI YA MKAA MBADALA KUPUNGUZA MATUMIZI YA MKAA NA KUNI

Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda (TIRDO), ikishirikiana na Taasisi ya n REPOA wamezindua mradi WA matumizi ya Mkaa mbadala, ambao unalenga kupunguza matumizi ya Mkaa WA Kawaida unatumia kuni, ikiwa sehemu ya kutimiza lengo la Mh Rais ambaye alitaka hadi kufika mwaka 2034, asilimia 80 Wananchi WA Tanzania wawe wameanza kutumia Nishati ya Mkaa mbadala.

Akizungumza kwenye mkutano na Waandishi wa habari hii Leo  Oktoba 7 2024, Mkurugenzi Mkuu (TIRDO) Prof Madundo Mtambo amesema kuwa katika kuhakikisha wanaunga mkono jitiahada za Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan wao kama sehemu ya Taasisi ya serikali inayojohusisha na maswala ya tafiti wameamua kushirikiana na REPOA ili kuhakikisha wanatimza lengo la kupunguza matumizi ya Nishati ya Mkaa kwa kutumia Kuni ambazo kwa miaka mingi imekuwa ikisababisha uharibifu wa Mazingira nchini.


Mtambo amesema Shirika la maendeleo ya viwanda nchini TIRDO, ambalo liko chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara, lillianzishwa mnamo mwaka 1979,ambayo ilianzishwa kwa mujibu wa Sheria  namba 5 ya Bunge ili kufanya utafiti na kutoa huduma za kitaalamu kwa maendeleo ya Viwanda Nchini

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya REPOA, Dkt Donald Mmari, amesema wao wanashiriki kwenye Mradi huo kutokana na wao kuwa ni watafiti wa maendeleo  ya kisheria kutokana na Shughuli mbali mbaliza Shughuli za kibinaadamu ambazo kulingana na tafiti zao wamebaini uharibifu wa Mazingira Kutokana na matumizi ya Nishati ya Mkaa, pomoja na Kuni.


 Aidha Mmari amesema kuanzia mwaka 2015,tafiti zinaonyesha upotevu wa misitu ambapo zimefikia kiasi cha hekta 3 72,000, ambapo miaka 7 baadae wamegundua ongezeko kubwa ambalo limefikia hekta 469,000 jambo ambalo ni hatari kwa Mazingira  ya nchini.

Kwa upande wake mmoja WA wakuu WA utafiti Bi. Kunda Sikazwe amesema Taasisi zote mbili zinawajibu WA kutatua changamoto kubwa ikiwemo zinazosababishwa na matumizi ya Nishati ya Mkaa na Kuni ambazo kitaalamu zinasababisha uharibifu mkubwa WA Mazingira lakini pia ni tishio kutokana na ukataji wa Miiti holela na kuharibu chanzo vingi vya Maji.

Aidha amesema kupitia Mradi huo huo wa pamoja wanaona wanakwenda kupunguza matumizi ya sasa ya Nishati ya Mkaa na Kuni huku pia akifafanunua unafuu unaopatikana kwa matumizi ya Mkaa WA sasa na Mkaa mbadala ambao Amesema Mkaa mbadala unapatikana rahisi mara 4 ya Nishati ya Mkaa na Kuni.




Powered by Blogger.