OFISI YA WAKILI MKUU WA SERIKALI NA TLS ZAINGIA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO YA KISHERIA
Na. Jumanne Magazi
Dar es salaam.
Wakili mkuu wa Serikali Dkt Ally Posi Amesema Serikali imedhamiria kuondoa kero zote zisizo na msing i kwenye mashauri yanayohusu mikataba na uwekezaji.Akizungumza wakati wa utiaji Saini makubaliabo baina ya Ofisi ya wakili mkuu wa Serikali pamoja na Chama cha wanasheria Tanganyika TLC uliofanyika Leo Septemba 25 2024 jijini Dar es salaam.Amesema makubaliano hayo yanalengo la kupeana ujuzi WA kitaalamu hususani maswala ya Sheria ili kusaidia Serikali na Wananchi katika changamoto za kisheria zinapojitokeza.Aidha amesema Ofisi ya a wakili mkuu ikishirikiana na chama cha wanasheria Tanganyika TLS, ushirikiano huo utakuwa na tija kwa Taifa katika maswala mbalimbali yanahusu taaluma ya Sheria huku akisisitiza Kuna haja kwa sasa watanzania kuanza kuamini wataaalam WA Sheria waliopo Nchini katika kutatua na kupunguza mlundikano WA kesi na mashauri hususani kwenye Mahakama zilizopo Nchini
Awali Rais wa chama cha wanasheria Tanganyika TLS, Boniface mwambukusi kwa upande wake amesema TLS wao kama wanasheria wamepongeza makubaliano hayo kwani yanalengo ya kuipinguzia mzigo Serikali na jamii kwa ujumla ambapo wakishirikiana na Ofisi ya wakili mkuu wa Serikali wataweza kuangalia mikataba ya uwekezaji ambayo nchi unaingia kwenye nyanja mbalimbali za Rasimali za nchi kwa maslahi ya Taifa kwa kizazi cha sasa na baadae
Makubaliano hayo yametanguliwa na kikao kazi cha ndani baina ya wataaalam WA Sheria WA Ofisi ya wakili mkuu wa Serikali pamoja na Chama cha wanasheria Tanganyika TLS.





Post a Comment