MATAIFA 33 YATHIBITSHA KUSHIRIKI MAONESHO YA UTALII SITE 2024 NCHINI
Na. Jumanne Magazi
Dar es salaam
Imethibitika kuwa Zaidi ya nchi 3 Kutoka kila pembeni ya Dunia zinataraji kushiriki Maonesho ya Kimataifa ya utalii yajulikanayo kama Swahili International Tourism Expro (Site) ambayo yamepangwa kufanyika kuanzia Octoba 11 hadi 13, 2024, Nchini Tanzania.
Akizungumza na Waandishi wa habari Jiji Dar es salaam Leo Septemba 24 2024, Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Ephraim Mafuru Amesema ,amesema uwepo maonyesho hayo, unalenga kukuza mtandao wa wafanyabiashara waliopo kwenye Sekta ya Utalii WA hapa nchini na Nje ya nchi.
Maonyeho hayo yanatoa fursa kwa Tanzania
Maonyeho hayo yanatoa fursa kwa Tanzania
Kuwa na uwezo wa kufikia masoko mbalimbali yahusuyo utalii ndani na Nje ya nchi hasa zile nchi ambazo hazileti watalii wake kwa wingi hapa nchini.
Mafuru Amesema tayari wamepokea uthibitisho wa ushiriki WA wadau 145 huku nchi Zaidi ya 33 zikithibitisha kushiriki Maonesho hayo ambayo yanaipa taswira kubwa nchini kwenye nyanja ya Utalii hapa nchini.
Aidha Mafuru amezitaja nchi ambazo tayari zimethibitisha kushiriki Maonesho hayo kuwa ni pamoja na
China, Denmark, Finland,Japan, Kenya, Africa kusini, Ethiopia india, Oman uholanzi Brazil Nigeria Ujerumani Uganda Lethoto na wenyeji Tanzania.
Miongoni mwa mambo yatakayozungumzwa kwenye mkutano huo kuwa ni pamoja na hali ya masoko ya Utalii Kimataifa, fursa za uwekezaji WA UTALII WA ndani na vivutio vingine vilivyopo hapa Nchini.
Post a Comment