MEYA MTINIKA ASAINI MKATABA WA UJENZI WA HOSPITALI MPYA YA WILAYA YA TEMEKE
Mstahiki meya wa manispaa ya Temeke ndugu Abdalah Mtinika ameshiriki zoezi muhimu la kusaini mkataba wa mwisho pamoja na kumkabidhi site mkandarasi wa ujenzi wa Hospital mpya ya Wilaya ya Temeke eneo la Vikuruti Chamazi ( maarufu eneo la Muhimbili.
Akizungumza wakati wa tukio hilo Mstahiki meya aliwahakikishia wana Temeke kuwa lengo la kusaini mkataba hadharani ni moja ya Hatua muhimu ya Uwazi na ushirikishwaji wa Jamii inayozunguka mradi huo ambao umesubiriwa kwa muda mrefuMstahiki meya ,Diwani wa Kata Chamazi mhe John Gama, viongozi mbalimbali pamoja na wananchi waliohudhuria kwa pamoja wametoa shukrani za dhati kwa Mh.Rais Dr.Samia Suluhu Hassan kwa Kuwajali wana Temeke kwa huduma za Afya.
Kazi inaendelea Temeke.
Post a Comment