JITOKEZENI MKAJIANDIKISHE KWENYE DAFTARI LA WAPIGA KURA: JAFO
31.8.2024
Mbunge WA Jimbo la kisarawe mkoani pwani Mh.Suleiman Jafo, amewahimiza Wananchi wa Jimbo Hilo na watanzania kwa ujumla kujitokeza katika kujiandikisha kwenye Daftari la wapiga kura.
Akizungumza kwenye kilele cha Tamsha maalum la Sana mtaa kwa mtaa lililofanyika mwishoni mwa mwezi uliopita.
Mheshimiwa Jafo amesema wakati Taifa likielekea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Vitongoji na mitaa Nchini unaotarajiwa kufanyika mwezi November mwaka huu ni haki ya kila mwananchi kujitokeza na kuhakikisha anajiandikisha kwenye Daftari Hilo ili Kujiandaa kwa ajili ya kushiriki Uchaguzi huo.
Aidha Jafo ambaye pia ni Waziri wa Viwanda na Biashara ametumia fursa hiyo kumpongea RAIS Dkt Samia Suluhu Hassan kwa judui zake katika kuwaletea maendeleo Wananchi Jimbo la kisarawe ikiwemo Maji, Elimu, afya pamoja na Umeme.
Awali akimkaribisha Mgeni Rasmi mkuu wa wilaya ya kisarawe Mheshimiwa Petro Magoti amesema kisarawe ya wakati huu imepiga hatua kubwa kimaendeleo chini ya muongozo WA Serikali ya Awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan, hivyo ameitaka jamii kumuunga mkondo mh Rais Katika harakati za kuhakikisha anipeleka mbele nchi katika nyanja mbalimbali.
Aidha Magoti ametumia hadhara hiyo kuwaalika wadau mbalimbali kushiriki kwenye TAMASHA kubwa la utalii wa ndani hususani kwenye wilaya ya kisarawe lijulikanalo kama KULA BATA MSITUNI 2024.
Tamsha ambalo limepangwa kufanyika kuanzia Septemba 22 2024 kwenye msitu wa Kazimzumbwi, Tamsha ambalo linalenga kutangaza vivutio vya utalii vilivyomo ndani ya wilaya hiyo huku mataifa Zaidi ya sita yakitaraji kushiriki Tamsha Hilo.
Post a Comment