WATUMISHI HOUSING KUPITIA FAIDA FUND KUFANYA MKUTANO WAKE WA MWAKA AGOSTI 10 MWAKA HUU
Akizungumza na waaandishi wa habari hii Leo AGOSTI 6 2024, Mkurugenzi Mtendaji wa Watumishi housing WHI, Fred Msema amesema.
Mkutano huo utafanyika kwa kuzingatia Sheria ya mamlaka ya masoko na Miraji (CMSA) ambapo kila mwaka WHI itakuwa ikiandaa mkutano huo, ili kutoa fursa kwa wanachama wao KUJADILI maswala mbalimbali yanayohusu mfuko pamoja na kupokea taarifa zenye maslahi kwa wawekezaji.
Akitaja faida na sifa za mfuko WA faida ambapo amesema mfuko huo ndio WA Kwanza Nchini kushusha kianzio cha kuweka kwa angalau kiasi cha Shilingi elf kumi 10000 Kwa kuanzia na wawekezaji wote iwe wadogo au wakubwa.
Vilevile amesema mfuko wao ndio mfuko pekee mwekezaji anaweza kuwekeza na kupata faida na kuchukua fedha zake bila kujaza fomu yoyote au kufika ofisini.
Naye Meneja Biashara Kutoka Bank ya CRDB, ambaye pia ndio wasimamizi na Muangalizi wa Mfuko huo.
Bi Mary Mponda ametumia fursa hiyo kuwataka Wananchi na wawekezaji kwa ujumla kuweendelea kutumia mfuko WA faida fund kuwekeza lakini pia kuwakaribisha wadau wote kupitia Watumishi housing kushiriki mkutano huo wa mwaka na amewaondoa hofu kuhusu Amana na fedha zao kuwa zipo salama.
Post a Comment