WANANCHI 3 KUIBURUZA TAMISEMI MAHAKAMANI KESHO
Na. Jumanne Magazi 27.8.2024
Wananchi watatu wazalendo DKT Ananilea NKYA, Bob Wangwe pamoja na Bubelwa Kaiza wamefungua kesi Mahakama kuu masjala ya Kanda ya Dar es Salaam, dhidi ya mwanasheria mkuu wa Serikali Kupinga Wizara ya Ofisi ya RaisTawala za mikoa na Serikali za mitaa (TAMISEMI) kusimamia Uchaguzi wa mwaka huu wa Serikali za vijiji, kamati za mitaa na Vitongoji.
Kwa mujibu wa TAARIFA iliyotolewa Leo Agosti 27,2024 na DKT Ananilea NKYA mbele ya Waandishi wa habari jijini Dar es salaam, kuhusu maombi hayo yatasikilizwa jumatano hii, Agosti 28 2024, ambapo awali maombi hayo yalitajwa kwa mara ya Kwanza Agosti 22, mwaka huu.
Aidha NKYA ambaye pia ni mwenyekiti wa jukwaa la katiba (JUKATA) amewaomba Wananchi kujitokeza kwa wingi kwa lengo la kusikiliza kesi hiyo ambayo itasikilizwa majira ya saa 8 mchana Mahakama kuu masjala ya Kanda ya Dar es salaam.
Kwa upande wake Bob Wangwe amesema kuwa wamefungua shauri Hilo, kwa kuwa wanatambua kwamba raia ndio mamlaka ya nchi kama inavyothibitishwa na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 8 (1) (a).Ameongeza kuwa "SISI raia kwa mamlaka tuliyonayo kwa mujibu na katiba tunapinga, na tunaona ni kinyume cha katiba na Sheria za nchi, iwapo TAMISEMI itasimamia Uchaguzi wa Serikali za vijiji,kamati za mitaa na wenyeviti WA Vitongoji.
Naye Bubelwa Kaiza amesema kuwa hatua hiyo ya kisheria unalenga kulinda haki ya kikatiba ya raia WA Tanzania kushiriki katika mchakato wa kedemokrasia ambao ni nyoofu, na huru na WA haki.
Post a Comment