TIGO NA ZMOTION ,WATOA MAFUNZO YA LIPA ADA KWA WAKUU NA WAMILIKI WA SHULE NCHINI


Na Jumanne Magazi 
27.8.2024.

Kampuni ya simu za   mkononi ya Tigo ikishirikiana  na ZMotion Leo hii  tarehe 27 Agosti 2024,kwa pamoja wametoa  Mafunzo ya Mfumo wa Malipo ya Ada kwa Wamiliki wa shule binafsi Tanzania bara.

Mkurugenzi wa Biashara-Tigo Pesa, James Sumari, Amesema  wao wakishirikiana na Zmotio
 "tumeendesha mafunzo ya siku moja kwa wamiliki na wakurugenzi wa shule binafsi  kuhusu huduma yetu mpya ya LIPA ADA"
Aidha amesema Mafunzo hayo yamefanyika, yakiwa na lengo la kuhakikisha ufanisi wa mfumo huo mpya ambao unatoa fursa kwa wazazi kulipia ada kidogo kidogo kulingana na uwezo wao.

 Sumari, ameeleza kuwa mfumo wa ‘LIPA ADA’ ni mojawapo ya ubunifu wa kiteknolojia uliolenga kutatua changamoto zinazowakumba wazazi na shule katika suala la ulipaji ada.
Sumari Ameongeza kuwa malipo kupitia mfumo huu yatakuwa yakifanyika kupitia huduma ya TigoPesa, hivyo kurahisisha mchakato mzima.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa ZMotion Said Ally alibainisha kuwa mfumo wa ‘LIPA ADA’ umesanifiwa kwa kuzingatia mahitaji ya shule binafsi na ni rahisi kutumia mfumo huo ambao utasaidia wazazi na walezi kwa ajili ya kufanya malipo ya ada kwa watoto wao.
Powered by Blogger.