TANZANIA KUWA MWENYEJI MKUTANO WA WADAU WA MAZINGIRA JIJINI DODOMA
Waziri WA nchi Ofisi ya Makamo wa Rais Muungano na Mazingira Mh Ashatu Kijaji amesema Tanzania inataraji kuwa wa mkutano mkubwa WA Sekta ya Mazingira utakao fanyika kuwanzaia Septemba 9-10 mwaka huu katika ukumbi WA Jakaya kikwete jijini Dodoma.
Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es salaam hii leo Agosti 27 2024 amesema mkutano huo unalenga kujadiri athari zinazotokana na matumizi ya NISHATI ya kaboni ambazo zinasababisha uharibifu wa Mazingira.
Mh Kijaji amesema Mkutano huo unararaji kukutanisha wadau Zaidi ya 1000 ambao wanatoka Sekta mbalimbali Kutoka Wizara na Taasisi za Serikali mashirika ya umma na watu Binafsi amesema katika mkutano huo wataangazia Zaidi matumizi ya Nishati ambazo zina hatarisha Mazingira.
Aidha amesema katika mkutano huo watajadiri na kuangalia fursa mbalimbali zilizopo katika hifadhi na usimamizi wa Mazingira ambazo zitainufaisha nchi kwa namna moja ama nyingine.
Vilevile mh Kijaji amesema madhumuni ya Mkutano huo ni pamoja na kujadili na kuweka mikakati mahsusi ya kukabiliana na changamoto za Mazingira ya nchi yetu.Pia mkutano huo unalenga kukuza na kupanua Biashara ya kaboni, usimamizi wa taka, Nishati safi ya kupikia, upandaji miti na usimamizi wa Sheria za nchi kuhusu Mazingira.
Aidha Mheshimiwa Kijaji ametumia mkutano huo wa Waandishi wa habari kumshukuru Rais DKT Samia Suluhu Hassan katika juhudi zake za kuhakikisha Mazingira yanakuwa salama kwa mustakabari WA nchi yetu.
Katika hatua nyingine Kijaji amewaomba watanzania na wadau WA Mazingira kuhudhuria Mkutano huo kwani una tija kubwa kwa nchi yetu.
Post a Comment