KATIBU MKUU FEMATA ASHIRIKI MKUTANO ULIOANDALIWA NA UMOJA WA MATAIFA


Katibu Mkuu FEMATA akiwa pia ni Mtoa elimu (Knowledge Exchange Coordinator) wa Mradi wa progamu ya Delve Exchange Coordinator upande wa Africa Swahili, inayosimamiwa na Bank ya Dunia chini ya Chuo Kikuu cha QueensLand cha nchini Australia, ameshiriki mkutano mtandaoni wa moja kwa moja uliandaliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres.

Mkutano huo uliratibiwa na Wenyeviti wenza wa paneli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ya Madini Mkakati (Critical Minerals), Balozi Nozipho Joyce Mxakato, balozi wa umoja wa mataifa  kutoka Afrika kusini na Balozi Ditte Juul Jorgensen ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Nishati Kamesheni ya Umoja wa Ulaya pamoja na Proffesa Daniel Franks kutoka taasisi ya kimataifa ya Sustainable Minerals.

Mkutano huo ulishirikisha mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa zikiwemo, UNEP, UNCTAD, UN TRADE, UNSG CAT na mengine, ulimshirikisha pia Mkhululi Ncube kutoka Umoja wa Africa(AU), Delve Exchnge Makao makuu pamoja na  watoa elimu wa Delve Exchange kutoka Africa English, Africa French, South East Asia Pacific, South Central Asia, Latin America,  pamoja na muwakilishi mwingine kutoka Tanzania ambaye ni mchimbaji Mecktilder Mchomvu.

Katika Mkutano huo Katibu Mkuu FEMATA akielezea nini kinachotakiwa kifanyike kwakuwa kuanzia mwaka 2025 madini yote yatatakiwa yaongezwe thamani nchini Tanzania kabla ya kusafirishwa nje ya nchi, aliiomba Umoja wa mataifa usaidie kwenye yafuatayo,

1. Umoja wa Mataifa usaidie uanzishwaji wa Benki ya Wachimbaji wadogo wa madini Tanzania itakayo tukopesha mitaji kutokana na mazingira ya uchimbaji wetu.

2. Umoja wa Mataifa usaidie upatikanaji wa Teknolojia rahisi na nafuu kwa mchimbaji mdogo, kuanzia utafutaji wa miamba, uchimbaji, uongezaji thamani mpaka kwenye kuuza na kusambaza madini. 

Na kwenye hili niiombe Umoja wa Mataifa usaidie Mradi ulioanzishwa na Wizara ya Madini wa Dira 2030 wenye lengo kufanya utafiti wa kina wa Madini nchini, utakaomsaidia mchimbaji mdogo kupata taarifa sahii za kijiolojia na aweze kuchimba kwa mafanikio.

3. Tunaiomba Umoja wa Mataifa usaidie kwenye mafunzo na elimu, kuanzia elimu ya utafutaji madini na miamba, elimu ya uchimbaji, elimu ya uongezaji thamani, elimu ya fedha, elimu ya utunzaji mazingira na elimu ya afya na usalama.

4. Tunaiomba Umoja wa Mataifa utusaidie kwenye kutuunganisha moja kwa moja na masoko ya Kimataifa ya madini yetu yatakayo ongezwa thamani ili tupate bei ya mtumiaji wa mwisho maana kwa sasa madini haya yana nunuliwa kwa wingi na watu wa kati au madalali ambao hutoza kamisheni na kumpunguzia faida mchimbaji mdogo.

5. Tunaiomba Umoja wa Mataifa utusaidie kuwezesha kupatikana wawekezaji wa ndani na nje  ya nchi pamoja na makampuni ya Kimataifa yatakayo wekeza nchini Tanzania kujenga Viwanda vikubwa vya uzalishaji bidhaa zinazotana na Madini Mkakati kama viwanda betri za lithium, Vifaa vya Umeme, Magari ya Umeme, Vifaa vya Umeme wa Upepo, Paneli za Sola na Simu janja, Makampuni haya yatatoa masoko kwa Wachimbaji wadogo, watatoa ajira nchini, watachangia uchumi wa nchi, watasaidia uongezaji thamani wa kiwango cha juu wa madini yetu na watasaidia upatikanaji na usambaaji wa teknolojia nchini ambapo wachimbaji wadogo watafaidika pia.

Powered by Blogger.