SAMIA KUZINDUA SGR DAR HADI DODOMA AGOSTI MOSI
Waziri wa Ujenzi na uchukuzi Mh Makame mbalawa amesema Serikali ipo tayari kuanza kutoa huduma ya usafirishaji abiria na mizigo kwa kiwango cha Kimataifa kupitia Treni ya Viwango SGR.
Shughuli nyingine ambazo zitaongezeka Kipato ni zile za Kijamii na Kiutawala, kwani SGR inatoa Usafiri wa uhakika na haraka.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania-TRC-MASANJA KADOGOSA amesema Serikali kupitia Wizara ya Uchukuzi imewawezesha kwa vitendea kazi, huku akiwahakikishia wananchi kwamba yapo Mabehewa ya kutosha.
Treni hiyo itakua na uwezo wa kubeba Mizigo hadi inayofikia Tani Elfu 10 kwa mpigo ambayo ni sawa na Malori Mia 5.
Post a Comment