KAMPUNI YA HEINEKEN BEVERAGES YAINUNUA BIA WINDHOEK SASA KUWA FAMILIA YA HEINEKEN
Na Jumanne Magazi.
Kampuni ya Heineken Beverages Limited imetangaza kufanya upanuzi WA soko lake la vinywaji vya Heineken Nchini Tanzania ambapo hii Leo Julai 31 2024 imetangaza kuinunua bia ya Windhoek inayotengenezwa na kampuni ya Namibia Breweries Limited,(NBL).Akizungumza mbele ya Waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Mabibo wine and spirits LTD. JeromeRugemalila,
ambao ndio wazalishaji na wasambazaji wa bidhaa ya Windhoek Tanzania amesema wameamua kuingia ubia na kampuni ya Heineken kwa lengo la kupunguza Gharama za uendeshaji kwa kile alichodai ni kuhadimika kwa dola jambo lililopelekea kupungua kwa UFANISI wao.
Aidha sambamba na hilo kampuni ya Heineken pia imetangaza ushirikiano wa Kimkakuni kampuni ya ki Tanzania ya Mabibo beer Ltd ambayo ni mzalishaji ambayo hapo awali ilikuwa na haki ya kulipekee kuagiza biavya Windhoek Nchini Tanzania.
Awali Meneja mkazi wa kampuni ya Heineken Beverages Tanzania Obabiyi Fagade amesema kitendo Chao kuinunua bia ya Windhoek Tanzania ni kuongeza soko la bidha zao kupitia bia hiyo ambayo imejitengenezea hapa nchini kwa miaka mingi.
Naye Meneja Masoko Kutoka kampuni ya Heineken Beverages Limited,Bi Lilian Pascal amesema kuanzia sasa bidha ya Windhoek itakuwa ikipatikaba Sambamba na bia ya Heineken popote pale nchini hivyo ushirikiano huo unararaji kuwa na matokeo chanya kwa siku za usoni.
Post a Comment