KISARAWE KUWA MWENYEJI WA TAMASHA LA KULA BATA MSITUNI 2024


Ofisi ya  Mkuu wilaya ya kisarawe imeandaa TAMASHA kubwa la burudani litakalojulikana kama "kula Bata Msituni 2024" ambalo litafanyika ndani ya msitu wa Kazimzumbwi uliopo minaki wilayani kisarawe 

Akizungumza na Waandishi wa habari mkuu WA wilaya ya kisarawe Petro magoti amesema TAMASHA Hilo Lina lengo la kutangaza vivutio vilivyomo ndani ya wilaya ya kisarawe, ikiwemo hifadhi ya msitu wa Kazimzumbwi.

Aidha magoti amesema jumla ya matifa 4 ya Africa mashariki yamesha thibitisha kushiriki TAMASHA Hilo ambalo litakuwa na mambo mengi ya burudani ikiwemo utamaduni WA kabila la mzalamo na aina mbali mbalimbali ya vyakula ikisindikizwa na  burudani mbalimbali

Katika hatua nyingine magoti amezitaja nchi zitakazoshiriki kuwa ni pamoja ana Uganda Kenya na wenyeji Tanzania, huku nchi zingi ne zikiendelea kuthibitisha ushiriki wao.

Tamsaha la kula Bata MSITUNI limepangwa kufanyika kuanzia Septemba 3 hadi 8 mwaka huu ambapo Zaidi ya wadau na wapenda burudani wapatao elf 3 wanataraji kushiriki TAMASHA Hilo la mwaka huu.

Powered by Blogger.