MAHUJAJI TANZANIA WAAGWA RASMI TAYARI KWA SAFARI YA HIJJA
10.05.2026
Dar es salaam
Zaidi ya mahujaji elfu 4000 watanzania wameagwa rasmi tayari kwa safari ya kwenda hijja katika miji ya Makka na Madina nchini Saudi Arabia, ambapo kundi la kwanza linataraji kuondoka Alfajiri ya jumatatu May 11 2026.
Ameyasema hayo leo,jumapili ya May 10,2026, katika makao makuu ya BAKWATA Taifa, jijini Dar es salaam, ambapo mbali na mambo mengine Nigeria amesisitiza swala la nidhamu na ukizingatia dhamira nzima ya safari hiyo.Aidha Ngeruko amesema imekuwa ni kawaida kwa baadhi ya mahujaji nchini kuwa na pupa na ghadhabu pindi mambo yanapokwenda ndivyo sivyo,jambo ambalo upelekea lawama na minong'ono kwa taasisi zilizowapeleka mahujaji
Naye Mkurugenzi wa Hijja na Umra Tanzania, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Shirikisho la Tanzania Haki Federation (TAHAFE), Haidary Kambwili amezungumzia maandalizi ya safari hiyo,ambalo amesema matayarisho yote yamekamilika ikiwemo swala ya Viza,vibali,tiketi na maswala mazima ya kiuhamiaji.
Aidha Kambwili ametumia fursa hiyo kuwaasa mahujaji wa Tanzania KWENDA kuwa mabalozi wazuri na kuwa taswira njema kwa TAIFA kwa kipindi chote watakapokuwa nchini Saudi Arabia.
Aidha Haidary amewaomba mahujaji kwenda Kuliombea Taifa na umma mzima wa watanzania Amani na Utulivu uzidi kuendelea na kusafisha Yale yote yaliyojitokeza siku za nyuma ambapo pia amewaomba kuwaombea Dua Viongozi wa nchi kuendelea kusimamia na kudumisha utawala Bora, ili nchi iendelee na Utulivu wake.
Naye mmoja wa mahujaji hao Sheikh Jalala Bin Juma ambaye amezungumza kwa niaba ya mahujaji Wengine amewaomba watanzania kuwaombea Dua wasafiri salama na warejee nyumbani salama, huku nao wakiahidi kuwaombea watanzania wote bila kujali dini na tofauti zao kuhusu amani na Utulivu wa nchi yetu.





Post a Comment