DIWANI NGATICHE: AKABIDHI PESA TASLIMU KWA WASHINDI,KUSOMA QUR AN MTAMBANI SEKONDARI

Na Jumanne Magazi 

10.05.2026

Dar es salaam 

Diwani wa kata ya Kinondoni Mh. Idrissa Said Ngatiche amekabidhi zawadi pamoja na pesa Taslimu kwa washindi wa Shindano la kusoma Qur an kwa makundi sita,katika shule ya Sekondari Mivumoni iliyopo kinondoni jiji Dar es salaam.

Akizungumza mara baada ya kukabidhi zawadi hizo MH Ngatiche ametumia jukwaa, hilo,kuwaasa Wanafunzi kushikamana na elimu ya dini na masomo ili kuwapa uwezo wakupambana na changamoto katika maisha.

Ameyasema hayo hii leo May 10,2026,ambapo mbali na mambo mengine amechukua fursa hiyo kuwapongeza walimu na uongo mzima wa shule ya Sekondari kwa juhudi kubwa kuwasomesha na kuwakaririsha Wanafunzi kitabu kitukufu Cha Qur an ambapo vijana wameonyesha uwezo mkubwa katika kuhifadhi kitabu hicho.

Aidha Diwani Ngatiche amekabidhi zawadi ya pesa Taslimu Shilingi Laki moja 100000/= kwa washindi 6, huku akitoa kiasi kingine Cha Tsh, elfu hamsini 50000/= huku washiriki wengine waliovutia watazamaji nao waliondoka na elf 50000/=.
Hii ni mara ya pili kufanyika kwa Shindano hilo ambapo kwa mwaka huu, zaidi ya Wanafunzi 36, washinda kwenye vipengele 4 ambavyo ni wale Waliohifadhi Juzuu 3 Juzuu 5, Juzuu 7, na Juzuu 15.

Naye mwalimu Mkuu wa shule Sekondari Mivumoni Tanu Kamaze amewashukuru wazazi na walezi kwa ushirikiano wao na viongozi wa shule hiyo jambo ambalo amelifananisha na samaki na maji, huku akiwataka kuendelea kuleta vijana wao kuja kusoma kitabu kitukufu mwenyezi mungu Cha Qur an tukufu.
















 

Powered by Blogger.