CHARLES MAKONGORO NYERERE ASHINDA TIKETI YA KUSHUHUDIA KOMBE LA DUNIA 2026 CANADA
Hatimaye Mh Makongoro Nyerere, mkuu wa mkoa wa Rukwa na mtoto wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage, ameshinda tiketi ya kwenda Canada kushuhudia mashindano ya Kombe la Dunia 2026 kupitia droo ya pili iliyofanywa na CRDB Bank.
Droo hiyo ni sehemu ya kampeni ya FIFA World Cup 2026: "Fainali Ndiyo Mpango na Tembo Card VISA", ambayo ililenga kuwapa washindi nafasi ya kushuhudia mechi za Kombe la Dunia katika nchi za Marekani, Canada, na Mexico. Kwa droo hii, washindi watatu walipata televisheni ya ukubwa wa inch 85, huku washindi wengine watatu wakishinda tiketi za kwenda Canada kushuhudia mashindano hayo.
Akizungumza kwa njia ya simu na CRDB Bank, Charles Makongoro Nyerere amewapongeza kwa kutoa huduma bora kwa wateja wao na pia kueleza furaha yake kuwa miongoni mwa washindi waliopata fursa ya kushuhudia tukio hilo kubwa la soka duniani.

Post a Comment