WANANCHI NYEBURU: WALIA NA SERIKALI UBOVU WA BARABARA UKOSEFU MAJI SAFI
Na Jumanne magazi
29.03.2026
Dar es salaam
Serikali imesema inaandaa mpango kazi utakao boresha miundombinu ya barabara pamoja na upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wa kata ya Buyuni na viunga vyake, ikiwemo mtaa wa nyeburu A,na B iliyopo katika Jimbo la Ukonga jijini dar es salaam.
Akizungumza na Wananchi kwenye mkutano wa hadhara, Afisa Tarafa wa Ukonga, Bw Kheri William, amesema serikali imepokea kilio na maombi ya Wananchi wa Mtaa wa Nyeburu kwa niaba ya wenzao wa Jimbo lote la ukonga, na kwenda kutatua changamoto kaubwa ya barabara pamoja na kuondoa kero ya muda mrefu ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama ndani ya Mtaa wa Nyeburu,pamoja na kata nzima ya buyuni.
Mapema kwenye mkutano huo mwenyekiti wa mtaa wa Nyeburu, Bw Sadati Athumani Rwetabula,aliiomba na kuishahuri Serikali kupitia taasisi zake ikiwemo Dawasco wakati ikisubiri miradi mikubwa ya muda mrefu kutekelezwa, kuchimba Visima vya dharula ambayo vitasaidia kupunguza makali ya ukosefu wa maji wananchi wa Nyeburu na viunga vyake.
Nao wananchi Zaituni Mohd Ali, Mohammed Omari Kitenge,wameupongeza uongozi wa serikali ya mtaa wa Nyeburu, hususani mwenyekiti na kamati tendaji yake,kuandaa mkutano huo muhimu uliowakutanisha wananchi na viongozi wa serikali akiwemo Afisa Tarafa kwani umeleta faraja kubwa kwa wananchi na wameomba kuwepo na utaratibu wa kufanya mikutano ya namna hiyo mara kwa mara







Post a Comment