MKURUGENZI,DIWANI: WAMSHUKIA MKANDARASI, KUCHELEWASHA UJENZI ZAHANATI BUYUNI

Na Jumanne Magazi

28.03.2026

Dar es salaam 

Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam Bw Bernard Kishamba amemtaka Mkandarasi anayejenga Wodi ya wazazi na jengo la upasuaji kuhakikisha jengo hilo linakamilika haraka na mapema. 

Ameyasema hayo leo March 28, 2026,Wakati wa ziara yake akimuakilisha Mkurugenzi wa Jiji la Dar es salaam maeneo ya Kata ya Buyuni Wilaya ya Ilala Jijini Dar es salaam.

Aidha Mradi huo ambao unatekelezwa kutokana na fedha za mapato ya ndani  (force account ) wenye thamani ya Shilingi 300Milioni zilizotolewa kwa ujenzi huo.
Kishamba, amesema"Ninasikitishwa na ucheleweshaji huu wakati pesa yote imeshatolewa. nimekuja lakini simuoni mkandarasi mwenye kazi hii. limenisikitisha sana hili linatia mashaka sana kwani fedha zimeshatolewa mapema lakini ujenzi bado unasuasua" amesema kaimu mkurugenzi 
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Buyuni Mh Jesca Mahmoud msolla, amemtaka Mkandarasi, kukamilisha jengo hilo, haraka kwani muda wa makubaliano ya mkataba wa awali umekwisha,ambapo alipaswa kukabidhi jengo march 30 mwaka huu, jambo ambalo amesema haliwezi kutekelezeka.
Aidha Diwani Jesca amemuomba Kaimu mkurugenzi huyo endapo Hali hiyo itaendelea kutokana na uzembe wa mara kwa mara wa Msimamizi wa idara ya masoko na timu yake kujitathmini vingievyo ameomba abadilishwe kutokana na kuchelewesha Kukamilika kwa mradi huo.

Mapema Mganga Mfawidhi wa hospitali ya buyuni Dkt Faraji Chivanga aliwasilisha,taarifa ya maendeleo ya ujenzi huo ambapo amesema mradi huo wenye thamani jumla ya Shilingi mil 300, umefikia hatua ya kenchi,huku tayari Ofisi yake imepokea kiasi cha Shillingi mil 300, ambapo Kati ya hizo milioni 129,921,865.6 zimeshatumika hadi sasa.

Mradi wa zahanati ya buyuni ulianza kujengwa mapema mwezi juni mwaka huu,baada ya halmashahuri ya jiji kuidhinisha kiasi Cha fedha milioni 168,ambazo zilielekezwa kukamilisha ujenzi huo kwa wakati


 

Powered by Blogger.