LIGU : AKABIDHI MSAADA KWA WATU WENYE MAHITAJI MAALUM,MTAA WA BWAWANI/MWANYAMAPA

Na Mwandishi wetu

Dar es salaam 

06.02.2026

Diwani wa Viti maalum kata ya mwananyamala,Salivina Gregory msulla alamarufu (Ligu) Amekabidhi msaada wa Chakula na mahitaji ya kibinaadamu kwa watoto kituo cha bwawani kilichopo mtaa wa bwawani kata ya mwananyamala, jijini dar es salaam.

Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo,Leo ijumaa 6 February 2026, Ligu amesema ni jambo jema kuona jamii ikiwakimbuka watu wenye mahitaji maalum hivyo wao kama KIKUNDI Cha vikoba wameona warejeshe kwa jamii kupitia makundi maalum.
Msaada uliokabidhiwa  ni pamoja na mafuta ya kupikia,sabuni,Michele, maharage, sukari ambapo jumla jumla ya wahitaji 50 walikabidhiwa msaada huo wakiwakilishwa na watu 10 kwenye makabidhiano hayo 

Aidha Ligu amesema amepokea maombi ya wanakikundi hicho, ambacho kinajishughulisha na biashara ya kukodisha viti na uuzaji wa vijora na Madera ya akina mama,huku wakiweka bayama changamoto yao kubwa ni kuwa ni ukosefu mitaji, jambo ambalo ameahidi kulichukua na kulifanyia kazi.

Naye Mlezi wa Kikundi hicho aliyefahamika kwa jina la mama Winne ameshukuru Diwani huyo kwa kukabidhi msaada huo kwa niaba Kikundi hicho, ambapo mbali na mambo mengine "amesema huwa wamekuwa wakifanya hivyo kila mwaka pindi wanapovunja kikoba hutenga fungu kwa jamii hususazi watoto yatima,wazee,wajane na wale wenye mahitaji maalum" amesema mama Winne mlezi wa Kikundi hicho.


 

Powered by Blogger.