SINGH MGENI RASMI MAHAFALI YA 45 DARASA LA SABA SHULE YA MSINGI YOMBO DOVYA, 2025

 


Aliyekuwa Diwani kata ya Keko 2020 - 2025 *Ndugu. Jasdeep Singh Babhra*  Mgeni rasmi katika mahafali ya 45 ya darasa la saba, Shule ya Msingi Yombo Dovya – Kata ya Makangarawe, Temeke.

Mahafali hayo yana akisi mafanikio na mageuzi Mazuri ya sekta ya elimu chini ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na *Mhe, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan,* kwa ushirikiano na Mkuu wa wilaya ya Temeke *Ndg. Sixtus Mapunda* na Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke *Ndg. Jomary Satura.* 

Shule hiyo imehitimisha wanafunzi 308 kwa ufaulu wa asilimia 95 kwa miaka minne mfululizo.

Hivyo Ndg Jasdeep Singh alitoa mchango wa fedha *Tsh milioni 1* kama motisha kwa walimu na wanafunzi, huku akisisitiza umuhimu wa kuendeleza Elimu, Maadili na Uzalendo kwa vijana, kama ilivyoainishwa katika Ilani ya CCM 2025–2030. 
Kata ya Makangarawe pia imenufaika na ujenzi wa Shule ya Sekondari ya kisasa yenye thamani ya *Tsh 2.8 bilioni,* ambapo tayari Mchakato wa Ujenzi umeanza.

SINGH alisema katika hotuba yake kuwa "Oktoba, tufanye maamuzi sahihi kwa maendeleo ya Temeke."


Powered by Blogger.