MWINYI AFUNGA MAFUNZO YA UONGOZI KWA VIJANA WA CCM DAR
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Ndugu Halid Mwinyi amefunga Mafunzo ya Uongozi kwa Vijana wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam yaliyohudhuriwa na Vijana zaidi ya 300 katika Wilaya ya Kigamboni jana Ijumaa 19 Septemba, 2025.
Katika hotuba yake, Mwinyi aliwakumbusha vijana nafasi yao katika uchaguzi huu ikiwa ni pamoja na kuendelea na kampeni katika makundi mbalimbali ya kijamii yaliyopo katika maeneo yao ili kuhakikisha 29 Oktoba wananchi wanakwenda vituoni kupiga kura za kishindo kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Wabunge na Madiwani wanaotokana na CCM.
Aidha, Mwinyi aliongezea kwa kuwataka vijana kutumia mafunzo waliyopata kuhakikisha wanaendelea kuwa chemchem ya fikra kwa vijana wenzao katika maeneo wanayoishi.
Vijana Tunasema Oktoba ni mwendo wa kutiki kwa Dkt. Samia kwa sababu ametuhakikishia fyucha bila stresi.
Post a Comment