IDRISSA NGATICHE: AZINDUA KAMPENI ZA UDIWANI KINONDONI KWA KISHINDO, AAHIDI MAKUBWA
*Aahidi kuendeza aliyoyaasisi, ikiwemo Afya, Barbara, elimu
*Ataja vipaumbele vyake 2025-2030
Kufungua Fursa za uchumi,kwa kujenga miundombinu ya Barabara,kutatua kero za wanakinondoni shamba
*Uwanja wa Garden mtambani kuwekwa taa, kufunga Taa za barabarani atenga fedha zake mfukoni kukamilisha baadhi ya miradi
* Asisitiza mikopo ya kinamama kutiliwa mkazo, ahidi kuleta wataalamu wa kibenki kuongeza elimu kwa wajasiliamai zikiwemo boda Bora mama lishe
* Asema ndani ya siku 100 atahakikisha anajenga mifereji ya maji kwa kushirikiana na viongozi wa serikali za mitaa kwa pesa zake mfukoni
Na jumanne Magazi20.09.2025
Dar es salaam
Mgombea udiwani kata ya Kinondoni kupitia chama cha mapunduzi CCM, Mheshimiwa Idrissa Said Ngatiche Leo hii amezindua rasmi Kampeni za udiwani kata ya Kinondoni, eneo la Kinondoni shamba.
Akizungumza na mamia ya wanachama wa ccm pamoja na wakaazi wa Kinondoni waliojitokeza kumsiliza amesema yeye anajua bado anadeni kubwa katika kuwaletea Maendeleo wakazi wa kata hiyoNgatiche amesema ndani ya uongozi wake wa miaka 5 iliyopita ameweza kufanya mengi ambayo kwa kipindi kifupi ameweza kuyatekeleza, ikiwemo ujenzi wa kituo cha Afya, ujenzi wa sekondari ya kata hiyo, pamoja na kusimamia ujenzi wa barabara ambazo zinajengwa chini ya mradi wa DMDP kwa kushirikiana na Halmashahuri ya Kinondoni.
Aidha Ngatiche amesema MAFANIKIO haya yoote yanaletwa na serikali ya ccm ambayo ndio yenye uwezo wa kuwaletea Maendeleo wananchi Kinondoni kupitia juhudi zake pamoja na mbunge wa Jimbo la Kinondoni.
Akisisitiza kuwa yale aliyoyafanya na atakayoyafanya ameweka wazi kuwa ndoto yake kubwa siku moja ni kuona kwamba kata ya Kinondoni inakuwa kama miji mikubwa Dunia ikiwemo london, kwa kuweka mazingira rafiki kwa wakazi jambo litakalowaletea Maendeleo Yao ndani ya miaka mitano ijayo.
Amesema "yeye ni mkaazi na mzaliwa wa Kinondoni hivyo changamoto zote za wananchi wa Kinondoni anazifahamu hivyo amewaomba Wana ccm na wananchi kumchagua yeye ili kumalizia kazi aliyoianza"Mbali na mambo mengine mgombea huyo ameahidi kushirikiana na wenyeviti wa serikali za mitaa ndani ya kata hiyo kuwaleta wataalamu watakao buni michoro na mipango ya kimkakati, ilikutatua Changamoto za barabara, mifereji ya maji jambo ambalo kwa muda mrefu amesema limekuwa changamoto kubwa kwa wakaazi wa Kinondoni shamba.
Aidha katika Kutekeleza hilo Mgombea huyo amesema ikibidi atatumia pesa yake mfukoni kusukuma juhudi za utakelezwaji wa Yale ambayo anaimani ndio kiu ya wanakinondoni.
Amuombea kura mgombea ubunge Jimbo la Kinondoni Mheshimiwa Tarimba Abas Gulam pamoja na Mgombea urais kupitia ccm Mhe Dkt Samia suluhu hassan
Kampeni hizo zitaendelea Tena Oct 4 Mwaka huu katika tawi la Kinondoni mjini eneo litafahamishwa hapo baadae.
Post a Comment