MTEULE UDIWANI KINONDONI CCM,ATAKA WANACHAMA KUUNGANA PAMOJA KULETA MAENDELEO YA KATA HIYO


Na. Jumanne Magazi 

Dar es salaam 

20.08.2025

Mteule wa ugombea udiwani kupitia chama cha Mapinduzi CCM, KATA ya Kinondoni, Idrissa Ngatiche amekemea baadhi ya  Wanachama na makada wa chama hicho,kuacha siasa za chuki fitna badala yake wavunje kambi na makundi yaliyokuwepo wakati zoezi la kura za maoni ndani ya chama hicho, badala yake waungane pamoja ili kuiletea Maendeleo kata hiyo, baada ya kupata ushindi kwenye uchaguzi mkuu ujao mwezi Oktoba.

Ameyasema hayo Leo Agosti 20,2025 muda mchache baada ya kukamilisha zoezi la urudishaji Fomu kwenye ofisi za mtendaji kata Kinondoni jijini Dar es salaam, ambapo amekiri kuwepo kwa kambi na Makundi miongoni mwa wanachama jambo ambalo limepelekea mpasuko miongoni mwa wanachama hicho.

Aidha Ngatiche amesema "nikweli Makundi ni jambo la kawaida kwa chama kikubwa kama CCM inapofika wakati wa uchaguzi wa ndani hususani kwa nafasi za uteuzi kuwepo kwa Makundi lakini yametupelekea kugawa chama na wanachama ccm jambo ambalo amesisitiza sio jambo jema.

katika hatua nyingine Ngatiche amesema chuki,ubinfsi,baina ya wanaccm ndani ya chama wamekuwa wakichukiana kutokana na sababu ambazo hazina msingi wala tija, kwa mustakabari mzima wa chama na wananchi kwa ujumla 

Vile vile mgombea huyo amesema muda umefika wa wanachama na chama hicho kuungana Pamoja na kusahau, yoote yaliyopita badala yake, waunganishe nguvu ili kukisaidia chama Cha Mapinduzi kupata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi mkuu ujao, na hatimaye kuwaletea Maendeleo wakazi wa KATA ya Kinondoni na maeneo yake 

Ngatiche ameteuliwa kuwa mgombea wa chama cha mapunduzi kupeperusha bendera ya ccm baada kuibuka mshindi kwenye kura zamaoni  ambapo sasa ataipeperusha bendera ya accm kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi mkuu ujao ambapo umepangwa kufanyika, mwezi Oktoba mwaka huu.

itakumbukuwa kuwa Idrissa anagombea uchaguzi huu ikiwa ni mara yake ya pili,baada ya kumaliza muhula wake wa kwanza kwa kipindi cha miaka 5 kwenye uchaguzi mkuu uliopita mwaka 2020.

 

Powered by Blogger.