TANZANIA YAWA MFANO AFRIKA UTEKELEZAJI MIRADI SEKTA YA NISHATI
Ufanisi wa utekelezaji wa miradi ya Sekta ya Nishati nchini ikiwemo ukamilishaji wa mradi wa usambazaji umeme katika Vijiji 12,318 umekuwa kivutio katika Jukwaa la Nishati Afrika linalofanyika nchini Afrika Kusinleta tokana na ufanisi huo unaojumuisha ukamilishaji wa mradi wa umeme wa Julius Nyerere wa megawati 2, 115 na baadhi ya miradi ya kikanda ya usafirishaji umeme, imepelekea nchi ya Lesotho kueleza nia yake ya kuja Tanzania ili kujifunza masuala mbalimbali yatakayoboresha hali ya umeme nchini humo.
Akizungumza katika Mkutano wa Jukwaa la Nishati Afrika jijini Cape Town nchini Afrika Kusini, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba ameeleza kuwa Watanzania wanapaswa kujivunia jinsi Sekta ya Nishati inavyofanya vizuri na kuwa nchi ya mfano barani Afrika.
Ametanabaisha kuwa, kutokana na hali ya ukuaji wa uchumi nchini, Tanzania kwa upande wake inaendelea kuongeza nguvu katika maeneo ya uzalishaji, usafirishaji na usambazaji umeme hivyo ushiriki wa sekta binafsi ni muhimu.
Post a Comment