KINONDONI TUNAJIVUNIA HATI SAFI MIAKA 4: MEYA SONGORO MNYONGE



Hatimaye Meya wa wilaya ya Kinondoni Songolo Mnyonge ameishukuru serikali ya awamu ya sita, kupitia ofisi ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG, kwa kuipa hati safi halmashahuri ya wilaya hiyo, kwa kipindi cha miaka 4 Mfululizo, jambo linawafanya wao kama madiwani kutembea kifua mbele kwa kipindi chotehicho.

Sambamba na hayo mnyonge ameipongeza  serikali kwa kuendeleza miradi ya maendeleo katika kata zote 20 za wilaya hiyo kwa kipindi cha miaka mitano, jambo linalowapa nguvu ya kutembea kifua mbele kwa wananchi wakati wakielekea kwenye uchaguzi mkuu ujao

Pongezi hizo amezitoa leo Jijini Dar es salaam wakati wa kuvunja baraza la madiwani katika wilaya hiyo amesema wanaondoka wakiwa mambo makubwa ya maendeleo iliyopelekea manispaa hiyo kuwa imara kwa utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi(CCM)

Katika kipindi cha miaka mitano yapo mafanikio mengi yaliyopatikana lakini mafanikio hayo hayakuja tu hivi hivi bali yalitokana na ushirikiano uliopo kati ya baraza la madiwa na serikali “,amesema 

Ameongeza kuwa mafanikio hayo pia yametokana na kusimamiana,kushirikiana na kuaminiana katika utekelezaji wa majukumu yao.

Sambamba na hayo Songolo amevipongeza vyombo vya usalama katika wilaya hiyo kwani wamefanya vyema kulinda amani na umoja kwa wananchi wa wilaya hiyo.

Tunajivunia umoja,amani na usalama katika wilaya yetu kwa kuwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama ambavyo ni imara”,amesema.

Sambamba na hayo Songolo amesema wameondoka wakiwa wameacha mambo makubwa yakiwemo magreda matatu yanayofanya kazi huku akitoa rai kwa mkurugenzi kuyasimamia lakini pia kurekebisha miundombinu iliyoharibika kutokana na mvua zilizonyeesha.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kinondoni Hanifa Hamza amesema mafanikio yaliyopatikana kwa kipindi chama mwaka 2020/2025 yametokana na mchango mkubwa wa baraza la madiwani.

“Baraza hili limekuwa na mchango mkubwa kwa maendeleo ya halmashauri yetu kuna miradi mbalimbali imetekeleza ikiwemo ujenzi wa jengo letu hili la halmashauri hivyo ni matumaini yangu kuwa baraza lijalo nitawaona wote kama mlivyo ili tuendelee kuiletea maendeleo kwa wananchi wa halmashauri yetu”,Amesema.

Sambamba na hayo amewaahidi madiwani hao kuwa miradi yote ya maendeleo inayoendelea ofisi yake itaisimamia vizuri na atatoa mrejesho kwenye baraza lijalo.

Naye,Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo amewapongeza madiwani hao kwa kutekeleza vyema irani ya chama hicho kama ilivyotakiwa.

 

Powered by Blogger.