PONDEZA: AKABIDHI SADAKA YA EID KWA WAHITAJI
Mwenyekiti wa Pondeza Foundation, Alhaj. Ussi Salum Pondeza amekabidhi sadaka ya chakula na fedha taslim kwa Yatima, wazee, wajane na wenye ulemavu wanaoishi jimbo la Chumbuni kwa ajili ya maandalizi ya Sikukuu ya Iddi.
Zaidi ya wananchi Mia tisa (900) wa jimbo la Chumbuni wamenufaika na sadaka hiyo
Pondeza ambae pia ni Mbunge wa wananchi Jimbo la Chumbuni ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi, Uenezi na Mafunzo CCM Zanzibar, Khamis Mbeto ambae alikua mgeni rasmi wa hafla hiyo amesema ni wajibu kwa viongozi kujitoa na kuwafikia wananchi wao kwani hatua hiyo inachangia upendo na mshikamano miongoni mwao.
Post a Comment