DIWANI KINONDONI: ATOA MKONO WA EID KWA WANAKINONDONI

Na Jumanne Magazi

Dar es salaam 

06.06 2025

Katika kile kinachonekana kurudisha hisani kwa jamiii yake, Diwani wa kata ya Kinondoni Idrisa Ngatiche said ametoa sadaka ya mkono wa idd baada ya kutoa ng'ombe 8 kama kitoweo kwa ajili ya siku kuu ya eid El adhha.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wakazi wa Kinondoni wamemshukuru Diwani wao kwa sadaka hiyo nakusema ni mtu ambaye anayaishi na kuyajua maisha ya wakazi eneo analo liongoza.

Seleman farahani mmoja wa waratibu wa zoezi Hilo amesema zoezi limekwenda vizuri huku akisisitiza zoezi Hilo lililenga kuwapa sadaka hiyo kwa wananchi na familia zenye huitaji zaidi jambo ambalo limetekelezwa kikamilifu.

Mwanaharakati na muhamasishaji na mkaazi wa Kinondoni Kado cool amezungumzia kwenye chapisho lake akimshukuru Diwani Ngatiche kwa kutoa nyama ya ng'ombe kwa baadhi ya wakazi waliojitokeza kwenye zoezi Hilo.

nipenda kumshukuru Diwani wa Kata ya Kinondoni Mheshimiwa Idrisa Said Ngatiche kwa kutoa Ng'ombe 6 kwa ajili ya wananchi wa mitaa 4 ya Kata yake na wadau wengine wa Kinondoni ili waweze kusherehekea sikukuu ya eid Al Adhwah

Kwa hakika ameonesha upendo wa hali ya juu kwa wananchi wake kuhakikisha wanaifurahia sikukuu ya kesho kwa upendo na amani bila ubaguzi wala upendeleo wowote"

"Lakini pia wananchi wa mitaa ya Kinondoni Mjini, Kinondoni Shamba, Kumbukumbu na Ada Estate, kupitia Viongozi wa Serikali za Mtaa  hiyo.

"Kado amesisitiza kuwa Kamati ilihakikisha inagawa kila Ng'ombe mmoja kwa mtaa husika, huku baadhi ya wadau wengine wa Kinondoni na maeneo mengin ya jirani"

Sikuu ya eid El adhwah huambatana na zoezi la kuchinja mara baada ya kukamilika kwa ibada ya hijja ambapo waumini wa dini ya kiislamu kote hukutana kwenye ibada hiyo ambayo hufanyika Makkah nchini Saudi Arabia.

Swala  ya eid Kitaifa kwa mwaka huu itaswaliwa katika msikiti wa Mohammed wa tano bakwata Kinondoni, ambapo mgeni rasmi anataraji kuwa Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh Kasim majaaliwa


 

Powered by Blogger.