MUSLIM HASSANNALI: ACHUKUA FOMU JIMBO LA KINONDONI
Na Jumanne Magazi
30.06.2025
Dar es salaam
Muslimu Hassanali amejiweka rasmi kwenye kinyang’anyiro cha ubunge kwa kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania Jimbo la Kinondoni katika uchaguzi ujao
Muslimu alichukua fomu hiyo katika ofisi ya CCM Wilaya ya Kinondoni, mkoani Dar es salaam, mbele ya viongozi wa chama hichoMuslim Hassanali anajiunga na orodha ya wanachama wa CCM wanaowania ridhaa ya kugombea ubunge kupitia chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu, huku Jimbo la Kinondoni likitarajiwa kuwa na ushindani mkali kutokana na mvuto wake wa kisiasa
Post a Comment