MASHIRIKA 14 KUUNGANISHWA ILI KULETA TIJA KWENYE GAWIO:MSAJILI WA HAZINA
Na Jumanne Magazi
02.06.2025
Dar es salaam
Msajili wa hazina amesema katika kuhakikisha pato la taifa linaongezeka serikali kupitia, ofisi ya msajili wa hazina inampango wa Kuunganisha mashirika ya serikali na baadhi ya taa sisi zake.
Akizungumza Wahariri na waandishi wa habari jijini dar es salaam hii leo 2 juni 2020/5.
Aidha Msajili wa Hazina ametoa taarifa RASMI kuhusu KUONGEZEKA kwa rekodi ambapo ongezeko la asilimia 40 katika makusanyo ya mapato yasiyo ya kodi ndani ya kipindi cha miezi 11, ikilinganishwa na kipindi kama hicho katika mwaka wa fedha uliopita.
Akizungumza katika kikao na wahariri wa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam siku ya Jumatatu, Juni 2, 2025, Msajili wa Hazina, Nehemiah Mchechu, amesema serikali imekusanya Sh884.7 bilioni kuanzia Julai 2024 hadi Mei 2025.
Hili ni ongezeko kubwa la mapato yanayokusanywa kutoka taasisi za umma na kampuni ambazo serikali ina umiliki wa hisa chache, ikilinganishwa na Sh633.3 bilioni zilizokusanywa katika kipindi kama hicho cha mwaka wa fedha 2023/24.
Pia hii inaonyesha ongezeko la asilimia 15.3 ikilinganishwa na jumla ya makusanyo ya mwaka mzima ya Sh767 bilioni katika mwaka wa fedha uliopita.
Mchechu amesema ukuaji huo wa mapato umetokana na kuimarishwa kwa utaratibu wa ufuatiliaji wa karibu wa gawio na michango katika Mashirika ya umma na matumizi ya Mifumo ya TEHAMA.
“Ofisi imefanikiwa kuunganisha Mfumo wa Mpango na Bajeti (PlanRep) na Mifumo ya ERMS na e-Watumishi pamoja na kufanya maboresho ya Mfumo wa MUSE ambao unawezesha kupata taarifa halisi za matumizi katika Taasisi na Mashirika ya Umma ili kuongeza uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa fedha za Umma,” amesema Mchechu.
Akivitaja vyanzo vikuu vya mapato kwa mwaka huu amesema ni gawio ambalo limechangia asilimia 63.9 ya mapato yote, huku michango ya asilimia 15 ya mapato ghafi ikichangia asilimia 29.7.
Aidha, mapato mengineyo yaliyojumuisha ziada, marejesho ya mikopo na riba pamoja na Mawasilisho yatokanayo na mtambo wa kuhakiki na kuwezesha mawasiliano (TTMS) yamechangia asilimia 6.4 ya mapato yote.
Mbali na kuongezeka kwa makusanyo ya mapato, pia uwekezaji katika kuimarisha utendaji wa watumishi wao kupitia viashiria muhimu vya utendaji (KPIs) umetajwa kuwa miongoni mwa mambo yaliyofanywa na Ofisi ya Msajili wa Hazina.
Akizungumzia siku ya gawio 2025, Mchechu amesema inatarajiwa kufanyika Juni 10, mwaka huu Ikulu jijini Dar es Salaam.
Amesema katika siku hiyo, taasisi na mashirika ya umma yatamkabidhi rasmi Mhe. Rais. Dk. Samia Suluhu Hassan, michango na gawio kwa Serikali.
“Tukio hili ni muhimu sana si tu kama alama ya uwajibikaji, bali pia kama chombo cha kutathmini utendaji wa mashirika na taasisi za umma kwa mujibu wa malengo ya Taifa,” amesema Mchechu.
Amesema Siku ya Gawio imekuwa kichocheo kikubwa cha mageuzi na mafanikio yanayooneka leo kwani tangu kuanzishwa kwa utaratibu huu wa wazi na wenye uwajibikaji, kumekuwa na ongezeko la mashirika yanayotoa gawio, pamoja na kuboreshwa kwa utendaji wao kwa ujumla.
Post a Comment