PURA: YAJIVUNIA MIAKA 4 YA DKT, SAMIA, SEKTA YA GESI ASILIA YAAHIDI MAKUBWA
19.05.2025
Mamlaka ya udhibiti wa mkondo wa juu wa Petroli (PURA),imesema inajivunia miaka 4 ya uongozi wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt Samia suluhu Hassan katika sekta ya gesi Asilia kwani imepata mafanikio makubwa.
Mkurugenzi mkuu wa mamlaka hiyo, Mhandisi Charles Sangweni amesema kuanzia marchi 2021 Hadi machine 2025,kiwango Cha gesi Asilia kilichozalishwa, kimefikia futi za ujazo bilioni 301.33.
Sangweni amesema kati ya kiasi hicho futi za ujazo bilioni 142.35,zilizalishwa kutoka kitaru Cha mnazi bay na futi za ujazo158.98,kutoka kitaru Cha songosongo.Ameyasema hayo Leo may 19 2025 jijijni dar es salaam,katika kikao kazi Cha wahariri na waandishi wa habari,chini ya usimamizi wa ofisi ya msajiri wa hazina (TR).
Mbali na mambo engine kikao hicho kimeangazia utekelezaji wa majukumu na mafanikio yaliyopatikana katika shughuli za utafutaji uendeshaji,uzalishaji wa mafuta na gesi Asilia chini ya serikali ya awamu ya sita.
Akifafanua zaidi, Mhandisi Sangweni amesema kwa kipindi cha nyuma, uzalishaji wa gesi ulikuwa ni wastani wa futi za ujazo,bilioni 32.03 kwa mwaka kwa upande wa mnazi bay huku, futi za ujazo bilioni 25.13 zilikuwa kwa upande wa songosongo.
Mhandisi Sangweni amesema PURA,inatekeleza majukumu yake kama yalivyoainishwa katika kifungu nambari 12 cha Sheria ya Petroli ya mwaka 2015.
Aidha PURA ilianzishwa ili kuleta mgawanyo mzuri wa majukumu kati ya mamlaka hiyo, na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).
Vilevile kusimamia na kudhibiti shughuli za mkondo wa juu wa Petroli , na kusimamia shughuli zote za miradi ya kusindika gesi asilia na hatimaye kuwa kimiminika.
Aidha Mhandisi Sangweni amesema lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha serikali inapata mgao stahiki kwenye mapato ya mafuta na gesi Asilia.
Post a Comment