WASHINDI 531 WA "MAGIFT YA KUGIFT " PAMOJA GARI 1 WAPATIKANA, DROO YA 8
03.01.2025
Hatimaye Kampuni ya mtandao wa Mawasiliano ya YAS, ikishirikiana na kitengo cha Mixx by Yas ,Leo hii January 3,2025, wamefungua mwaka kwa kukabidhi zawadi mbalimbali kwa washindi wa Shindano la “Magift ya kugift” kwenye DROO 8, akiwemo mshindi WA gari aina ya Kia 0.km
Aidha washindi hao wamejishindia kiasi cha Shilingi Milioni 1 kila mmoja
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo kwa washindi Mkurugenzi wa masoko, Kutoka YAS, Edwadina Mgendi, amesema anayofuraha kuona wanakabidhi zawadi kwa washindi wa droo ya nane 8 nakudai kuwa hii ni sehemu ya utaratibu wao kutoa zawadi mbalimbali ikiwemo pesa taslimu na zawadi nyinginezo katika kipindi hiki cha kuelekea siku kuu za mwisho wa mwaka.
Mgendi amesema mpaka sasa wameshatoa zawadi za fedha zenye thamani ya kiasi cha TSh milion 244, kwa washindi wa makundi tofauti ikiwemo,mawakala,na wateja wengine.Kwa upande wao, washindi wa wiki hii, Agnes Michael Najua na Said Rashid Athumani wakiwakilisha wenziwe ambaye amejinyakulia kiasi cha Shilingi mil 1, “amemshukuru Yas kwa kuchezesha kampeni hiyo yaj "MAGIFT ya KUGIFT 2025" na hatimaye yeye kuibuka mshindi, na amewaomba watanzania kushiriki kampeni zinazoletwa na Yas Tanzania kwani hakuna ubabaisha kila mtu anashinda kutokana na bahati yake amesema Agnes.
Kampuni ya YAS imekuwa na muendelezo mzuri WA kuendesha kampeni mbalimbali ikiwa sehemu ya kujitangaza itakumbukwa kuwa kampuni ya YAS ilizinduliwa hivi karibuni ikichuka pahala la Tigo ambayo imedumu kwa kipindi cha miaka 30 ikitoa huduma zake hapa nchini, na kutunukiwa Tuzo mbali mbali ndani na Nje ya nchi, ikiwemo Tuzo ya mtandao wenye Kasi Zaidi Barani Africa inayotolewa na OOKLA, mwishoni mwa mwaka Jana
Hii ni wiki ya Saba mfulululizo kati kati ya wiki 12 ambazo Yas kupitia msimu huu wa siku kuu, ikishirikiana na kitengo cha Mixx by Yas, imeendelea kutoa zawadi Zaidi kupitia kampeni Yao ya "Magift ya kugift" kwa wateja wao kwa mwaka huu wa 2025.
Post a Comment