SHIRIKA LA WOMEN TAP YAWAGUSA WANAWAKE.
Shirika la Tanzania Women Tapo kwa kushirikiana na Hospitali ya Aga Khan wamezindua rasmi Kampeni ya Afya kwa Wanawake wa Masokoni na Wachuuzi, mpango uliolenga kuwafikia wanawake wapatao 31,000 katika mikoa yote 31 ya Tanzania.
Akizungumza leo mapema jijini Dar es Salaam wakati wa Uzinduzi uliofanyika Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania Women Tap,Lulu Nyapili,amesema kampeni hii inalenga kutoa huduma za uchunguzi wa afya, elimu ya kifedha, na uhamasishaji wa masuala ya kijamii kwa wanawake wa masokoni na wachuuzi, ambao wanatajwa kuwa mhimili muhimu wa uchumi wa taifa.
“Hawa si wauzaji tu, bali ni wajasiriamali, mama, na viongozi wa jamii. Kampeni hii siyo tu mpango wa afya, bali ni matumaini na mabadiliko,” amesema.
Nyapili amesema changamoto nyingi zinazowakabili wanawake huku juhudi zinaendelea kuhakikisha wanapata heshima na msaada wanaostahili.
“Wanawake hawa wanahitaji kuonekana, kusikika, na kuthaminiwa,” ameongeza Mkurugenzi.
Mkurugenzi huyo ametoa wito wa dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kushirikiana katika kampeni hii na kukutana na wanawake hao ili kusikiliza changamoto na ndoto zao.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Mganga mkuu Mkoa wa Dar Es Salaam,Ayoub Kibao,ambaye ni Mratibu wa Huduma za Ukimwi mkoani hapa,amesema serikali inatambua mchango wa Afya wanawake kwani bila afya ya wanawake Taifa haliwezi kupiga hatua.
Kwa Upande wake,Mkurugenzi wa Taasisi ya huduma Afya Aga Khan,Sisawo Konteh,amesema makubaliano na taasisi hizo yanalenga kuwasaidia wanawake wa kitanzania kimatibabu.
Post a Comment