TRC: SGR KUANZA KUTOA HUDUMA YA USAFIRI WA MIZIGO HIVI KARIBUNI
Na Jumanne Magazi
16.1.2025
Shirika la Reli nchini TRC, limesema lipo kwenye mchakato ili kuanza kutoa huduma ya usafiri wa mizigo kupitia treni yake ya mwendokasi SGR hivi karibuni.
Akizungumza na Waandishi wa habari mapema hii Leo 16. Januari 2025, Mkurugenzi mkuu wa TRC, Masanja Kungu Kadogosa amesema Mabehewa ya mizigo yameshaingia Nchini tayari kuanza kutoa huduma ya usafiri wa mizigo.
Kadogosa amesema Mabehewa ya mizigo yanatarajiwa kuanza kusafirisha bidhaa kupitia Reli ya Standard Gauge Railway (SGR) ndani ya miezi miwili ijayo kwani tayari matengenezo ya miundombinu yamekamilika.
Kadogosa amesema kuwa serikali inatarajia kupata faida kubwa kutokana na usafirishaji wa mizigo kupitia SGR, na kwamba tayari wafanyabiashara wameonyesha nia ya kuanza kutumia huduma hiyo na wengine tayari wameomba kuanza kupokea mizigo Yao kutoka Dodoma.Amesema kuwa serikali imejipanga kikamilifu kutatua changamoto zinazoweza kujitokeza katika usafiri wa SGR.
"Changamoto zipo, lakini serikali imejizatiti kuhakikisha kuwa zinashughulikiwa haraka, na endapo itajitokeza hali ya treni kusimama njiani, marekebisho yatafanyikaharaka sana ili abiria waweze kuendelea na safari zao bila kupoteza muda.
Kwa Sasa changamoto kubwa inatokana na mvua inaponyesha zile sehemu zilizokuwa zimeharibiwa kipindi Cha nyuma na wezi Wa mitambo ya SGR maji yanapoingia yanasababisha hitilafu lakini Kwa Sasa tatizo Hilo linaendelea kushughulikiwa" amesema Kadogosa.
Aidha ameongeza kuwa Katika kipindi Cha miezi minne watu millioni 1.4 wamesafiri Kwa treni ya SGR ambapo Kwa siku watu 5,000 mpaka 10,000 husafiri Kwa treni ya SGR.
Post a Comment