MIL. 10 ZA "MAGIFT YA KUGIFT" ZAENDA TANGA, KWA ATHUMANI MRISHO

Na. Jumanne Magazi

Hatimaye Kampuni ya Mawasiliano ya Yas Tanzania Leo hii Jan 7, 2025 imekabidhi zawadi ya Tsh Mil 10 kwa mshindi WA Droo 9 ya promosheni ya "Magift ya Kugift” kwa mshindi Athumani Mrisho Kutoka mkoani Tanga.

Kwa upande wake Meneja Mauzo wa Yas Mkoa wa Tanga Amani Sailoja amempongeza, mshindi , huyo Kutoka Wilayani Mkinga, ambapo mbali na mambo mengine amesema ametumia hafla hiyo kuwataka wateja wengine WA Mixx by Yas pamoja na Yas Tanzania kuendelea kushiriki Promoshe hiyo kwani kila mmoja ana fursa ya kujishinda zawadi hizo.

Meneja mauzo wilaya ya Muheza   Telly Maile, pamoja na. Meneja wa Biashara na masoko wa kampuni  hiyo Pwani ya kaskazini mkoani humo Mohamed Bagasha kwa pamoja wametumia hafla hiyo, kuwashukuru wateja WA Yas kwa kuendelea kutumia mtandao huo,ikiwemo kufanya miamala ya mara kwa mara na hatimaye kujishindia zawadi Kutoka Magift ya Kugift.


Kwa upande wake Mshindi wa Mil 10 Bw Athumani Mrisho, amesishukuru YAS kwa zawadi hiyo ambayo amesema inakaenda kubadiri maisha yake,baada ya kushinda hivyo amewataka wateja wengine kuendelea kushiriki kwa kufanya miamala ya mara kwa mara na wao ili waweze kujishindia zawadi kama ilivyo kuwa kwake 

Kampuni ya YAS Tanzania imekuwa Ikiendesha promosheni hiyo, kwa muda WA wiki 12 ambapo hadi kufikia Leo zaidi ya kiasi cha Shilingi Zaidi ya mil. 250 zimeshatolewa zikienda kwa  washindi mbalimbali  sambamba na zawadi hizo zikiwemo simu za mkononi

 


 

Powered by Blogger.