CCM :Kuchanua maendeleo zbar vigogo ACT taaban


 Na Mwandishi Maalum ,Zanzibar

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimelaani na kukiita kitendo cha ACT Wazalendo kutangaza takwimu feki za mikopo na madeni ya ndani na nje na kudai Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) inadaiwa trilioni 3.6 ni siasa za kijuha.

Pia kimesisitiza hakuna deni la Trilioni 3.6 badala yake SMZ deni lake la ndani ni trilion 1. 2 pekee kinyume na propaganda hasi za upinzani 

Maelezo hayo yametolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar,Idara ya Itikadi , Uenezi na Mafunzo,Khamisi Mbeto Khamis , kufuatia kusambazwa kwa taarifa ya ACT iliodai SMZ ina deni la Trilioni 3.6346

Mbeto alisema ACT na Watalaam wake kwanza wameshindwa kutofautisha na kutojua maana ya deni la ndani na nje, hivyo juhudi zao zote ni kutaka kujenga imani kwa wanachama wao , kupata umaarufu wa kisiasa huku wakiropokwa maneno ya kujifariji.

Alisema kwa mujibu wa dola ya tanzania ni .moja , Zanzibar haina deni la kitaifa wakati kuna Jamhuri ya Muungano ni moja, na Zanzibar haina vyeti vya kukopa nje bila kibali cha serikali ya Tanzania. 

'Chachu na kushamiri kwa maendeleo yanayoonekana sasa Zanzibar vigogo wa ACT wako taaban . Hawana la kuwaambia wanachama wao hadi wakaridhike kuelekea oktoba mwaka huu. Hoja zao za kisekta zimefyonzwa na ufanisi na kupotezwa na utendaji wa SMZ " Alisema Mbeto 

Aidha Mwenezi huyo aliongeza kusema mikopo na madeni ya nje ni dhamama ya Serikali ya Muungano hivyo Zanzibar ina kibali cha kukopa mikopo ya katika taasisi za ndani za fedha si mikopo ya kimataifa .

"Tunajua upinzani maji yamewafika kooni. Wamevurugwa na msisimko wa maendeleo yaliochanua Unguja na Pemba chini ya Rais Dk Hussein Mwinyi . Upinzani umefilisiwa hoja zote. Viongozi ACT wameamua kutunga uongo ili kuwapoza vichwa wafuasi wao " Alieleza 

Mbeto aliesema hadi sasa kwa mujibu wa takwimu za Fedha kwa madeni ndani, SMZ deni lake ni himilivu hivyo SMZ bado inakopesheka , hata ikitaka kesho kukopa itakopeshwa na wala si kweli kila mzanzibari kama ana deni.

Katibu huyo Mwenezi ,alisema ni aibu kwa viongozi ACT kuonekana wakiishangaa SMZ kukopa fedha wakati kazi kubwa ya kusukuma mbele maendeleo ya kiuchumi na huduma za jamii imefanyika na kuonekana na kila mwananchi.

"Kinachofanywa na vigogo wa ACT ni kupapatua ili waonekane wapo na wanasema hata kama wanayoyasema hayawaingii akilini wananchi. Kwakuwa wapo katika siasa wanaona heri waonekane wapo wapo na kusema ili wasikike "Alisema 

Pia Mbeto alieleza kwa miaka yote baadhi ya wanasiasa wa upinzani wanapinga Muungano wa serikali mbili, sababu za kufanya hivyo imebainika ni kuizuia Zanzibar isifaidike na mikopo ya nje itokanayo kibali cha serikali ya Tanzania ,wakati huo huo SMZ ikikopa mikopo ya ndani .

"Hakuna Taifa hata moja duniani linaloweza kusema halikopi au halina deni kwa maendeleo ya watu wake. Act wasifikiri kazi ya kuleta maendeleo ya nchi kama ya kucheza lelemama ,mbwa kachoka au beni bati" Alisema

Akijibu madai ya kukosekana uwajibikaji ,ufanisi na uwazi , Mbeto alisema bila ya ufuatiliaji wa karibu wa SMZ katika sekta za maendeleo, utekelezaji wa miradi mikubwa isingekamilika kwa viwango na wakati. 

"Sisi CCM kadri tunavyofuatilia kazi za Serikali yetu ili tujiridhishe tumekuwa tukivutiwa na kasi ya uwajibikaji wa kila sekta. Jukumu la kwanza la kusimamia miradi ya maendeleo ni la CCM yenye Ilani ya Uchaguzi kabla ya watendaji wa SMZ " Alifafanua Mbeto 

Hata hivyo Mwenezi huyo alisema tokea kuingia vyama vingi, upinzani ulikuwa ukikosoa urasimu unaozorotesha utendaji wenye ufanisi katika baadhi ya sekta,lakini kwa kuwepo usimamizi makini na utekelezaji wa kisera, upinzani umepoteza mvuto na hoja za mashiko.

Powered by Blogger.