MHANDISI MAHUNDI ACHANGIA 2M KIKUNDI CHA VICOBA IVIMA MAKONGOLOSI

Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya amechangia shilingi milioni mbili kwa kikundi cha VICOBA Ivima cha Makongolosi Wilaya ya Chunya Mkoani Mbeya kwa ajili ya ukamilishaji wa ukumbi wa mikutano.

Mbali ya kuchangia pesa hiyo Mahundi amekipongeza kikundi hicho chenye wanachama thelathini kwa namna kinavyopiga hatua kwa kuwa na miradi mingine kama kioski cha maji na maduka
Awali Besta Masika katibu wa Kikundi hicho amesema wanahitaji shilingi milioni hamsini ili kukamilisha ujenzi wa ukumbi huo utaosaidia ufanyikaji wa mikutano kwa wakati.

Masika amesema changamoto inayowakabili ni pamoja na baadhi ya wanachama kutorejesha mikopo kwa wakati.









Powered by Blogger.